Fahamu kila kitu Kuhusu VPN na matumizi yake

 


VPN NI NINI?


VPN ni kifupi cha Virtual Private Network. Ni encrypted tunnel kati ya vifaa viwili ambayo inakuwezesha kuingia kwenye kila website na huduma nyinginezo za mtandaoni privately na securely.


SAWA, SASA HII VPN TUNNEL INAFANYAJE KAZI?


VPN tunneling inaunda point-to-point connection baina ya vifaa viwili, mara nyingi inakuwa ni VPN server na kifaa unachotumia wewe. Tunneling ina-encapsulate data zako kwa mfumo wa standard TCP/IP packets na unazisafirisha kwenye internet kwa usalama kabisa. Kwasababu data ziko encrypted, wadukuzi (hackers), serikali (governments), hata ISPs (Internet service providers) hawawezi kuona au kuzipata taarifa zako kipindi chote unachokuwa umeunganishwa kwenye VPN server.


OH OK. LAKINI KWANI VPN INA UMUHIMU GANI KWANGU?


1. Unataka kuwa 'private'?

Kama hutumii VPN, basi upo uchi. Yule anaekuwezesha kupata huduma ya internet (ISP) anaweza kuona internet traffic yako na huenda akawa ana kumbukumbu zako za vitu vyote unavyofanya mtandaoni.


2. Unachukia 'censorship'?

Ni mara ngapi umeingia kwenye website fulani au huduma fulani mtandaoni halafu ikakwambia - "This service is not available in your country". Hiyo ndo censorship sasa, na huwezi kuiondoa bila VPN.


3. Okoa pesa wewe!

Kuna baadhi ya online stores huwa zinatoza bei ya bidhaa kutokana na 'location'uliyopo. Yaani, kama upo Canada unapata punguzo la hadi 50% wakati kama upo Africa unauziwa kwa bei halisi na shipping costs juu! Ubaguzi wa namna hii huwezi kuushinda bila VPN.


4. Encrypt kila kitu.

Hackers sio watu wazuri, huwezi jua ni saa ngapi wanakuwinda hasa hasa kama wewe ni mzee wa kupenda Kitonga, a.k.a Public Wi-Fi. Wadukuzi wanaweza wakapita na taarifa zako nyeti. Sasa kabla hawajakushika pabaya, tumia kinga - VPN.


ANHAA SAWA. NA JE, VPN INA UTOFAUTI GANI NA PROXY?

Ukiwa connected kwenye PROXY SERVER, inakuwa ni kiunganishi kati ya kifaa unachotumia na internet. Traffic yako yote inapitishwa kwenye proxy server, na hivyo itaonekana kama imeanzia kwenye IP address ya proxy server. Proxy server inakuficha/ inaficha IP address yako na kukuruhusu ku-access maudhui yaliyozuiwa. Hata hivyo, proxy server hai-encrypt traffic yako, kwahiyo taarifa unazotuma na kupokea zinaweza kudakwa/ kuingiliwa na mtu yeyote hususani wadukuzi na ídentity thieves.


VPN inakupa kila ambacho unapata kwenye proxy servre lakini pia inalinda na kufanya encryption ya data kati ya kifaa unachotumia na internet, hivyo inakupa ujasiri wa kutumia mtandao pasipo hofu ya taarifa zako kuvuja.


SAFI. NA VIPI KUHUSU FIREWALL, INATOFAUTIANAJE NA VPN?

Firewall ni kizuizi kinachochambua 'data packets' kutoka kwenye mtandao ambazo zinajaribu ku-connect na computer yako na kinaruhusu data packets zile ambazo zimekidhi vigezo ambavyo vimewekwa tu. Kutumia firewall ni njia nzuri ya kulinda kifaa unachotumia dhidi ya hatari mbalimbali kama vile virus attacks na worms. Hata hivyo, firewall inakulinda na traffic inayoingia kwenye kifaa unachotumia tu (Incoming traffic). Traffic inayotoka hailindwi na firewall, hapo ndipo unapohitaji VPN. Ukitumia vyote viwili inakuwa upo salama zaidi.


AISEE! MALIZIA KWA KUTUELEZEA TOFAUTI YA VPN APP, VPN PLUGIN NA VPN BROWSER

VPN browsers au browser plugins zinalinda WEB BROWSER TRAFFIC tu!. Network traffic nyingine yote kutoka kwenye kifaa unachotumia inabaki uchi, watabe wanaweza kuichungulia. VPN app yenyewe ndo inaweza ku-encrypt na kulinda 'network traffic' kutoka kwenye kifaa chako. Kwahiyo ukitaka uwe salama, usitumie Browser plugin peke yake, tumia app.



0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa