Baada ya mtandao wa Facebook kuleta sehemu ya Delete For All kupitia App ya WhatsApp, hivi karibuni mtandao huo uko njiani kuleta sehemu mpya kupitia app yake ya Facebook Messenger itakayo kuwezesha kurudisha meseji uliyokosea kutuma.
Kama ilivyo kwenye WhatsApp,  kupitia sehemu hiyo pia itakuruhusu kufuta meseji uliyokosea kutuma ambapo meseji hiyo itafutika kwa upande wako, na pia kwa kutumia sehemu ya “unsend” meseji hiyo itaweza kufutika kwa uliyemtumia pekee.

 Kupitia sehemu hiyo pia utaweza kufuta meseji ulizokosea kutoka mda machache tokea utume meseji hizo, hivyo utaweza kurudisha meseji ambazo zimekaa kwa muda mrefu sana. Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu lini sehemu hii itakuja kwenye App ya Messenger hivyo hakikisha unaendelea kutembelea Swahili Tech tutakujuza zaidi kuhusu sehemu hii.
Axact

Ibrahim Riyad Houmud

As Salaam Aleikum, I'm Ibrahim Riyadi Houmud, Founder and CEO of RiyadiBhai blog from Mororgoro, Tanzania. I started this blog as a Passion and it now empowering thousands of readers around the globe.Here I usually share news, Adsense tips, wordpress, gadget, widget, Themes, windows, etc.

Post A Comment:

0 comments:

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa