Waanzilishi wa Mtandao wa Instagram Waachana na Facebook

Mtandao wa Instagram ambao kwa sasa unamilikiwa na kampuni ya Facebook ulianzishwa mwaka 2010 na waanzilishi Kevin Systrom na Mike Krieger, toka kipindi hicho mtandao wa Instagram umekuwa kwa kasi hadi kufikia mwaka 2012 ambapo Facebook ililipa dollar za marekani bilioni $1 kwaajili ya kununua mtandao huo.
Baada ya Facebook kununua mtandao huo, mtandao wa Instagram umeendelea kukuwa kwa kasi hadi kufikia kiasi cha watumiaji zaidi ya bilioni 1. Kwa kipindi chote hicho waanzilishi wa mtandao huo Kevin Systrom na Mike Krieger waliendelea kufanyia kazi mtandao huo wa Instagram lakini ikiwa ni chini ya kampuni ya Facebook.
Sasa habari za hivi karibuni kutoka kwenye mitandao mbalimbali zinasema kuwa, waanzilishi wa mtandao wa Instagram Kevin Systrom na Mike Krieger wametangaza kuachana rasmi na mtandao wa Facebook, taarifa hizo zilizuka hapo siku ya jana na kutangazwa rasmi kupitia mtandao wa New York Times. Hata hivyo baadae taarifa hizo zilidhibitshwa kwa taarifa maalum iliyotolewa na mmoja ya waanzilishi hao kupitia mtandao huo.
Kupitia taarifa hiyo iliyotolewa na Kevin Systrom kwenye blog ya habari ya Instagram, Systrom ameandika kuwa “Tunatarajia kuchukua muda mwingi kuchunguza udadisi wetu na ubunifu wetu,” aliandika. “Kujenga mambo mapya inahitaji sisi kurudi nyuma na kuelewa nini kina tuhamasisha na pia kitu hicho kiendane na mahitaji ya dunia; ndio tunachotaka kufanya.” aliandika Systrom muanzilishi mwenza wa mtandao huo wa Instagram.
Hivi karibuni waanzilishi wengine wa programu ya WhatsApp kwa nyakati tofauti waliatangaza kuachana na kampuni ya Facebook, huku mmoja wao akitangaza kuachana na kampuni hiyo mara baada ya kutofautiana na kampuni hiyo juu ya uendeshaji wa mtandao wa Facebook na WhatsApp kwa ujumla kwa kile kilichosemekana kuwa ni kutokuzingati sera za faragha za watumiaji wa programu ya WhatsApp pamoja na Facebook kwa ujumla.
Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti mtendaji na mwanzilishi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg aliandika kwenye maelezo yake kuwa “Nimejifunza mengi kufanya kazi nao kwa kipindi cha miaka sita na nimefurahia sana. Ninawatakia mema wote na ninatarajia kuona kile watakachojenga baadaye. ” alisema Mark baada ya kupokea taarifa ya waanzilishi wa mtandao wa Instagram kuacha kazi kutoka kwenye kampuni yake.
Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi juu ya nani atakaye shikilia nafasi za wabunifu hao baada ya wabunifu hao kuachana na mtandao huo ndani ya wiki mbili zinazokuja ila kwa taarifa zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Swahili Tech kila siku.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa