Vodacom Yarahisha Manunuzi Mtandaoni kwa M Pesa Card

Idadi ya watumiaji wa teknolojia inazidi kupanda kila siku, vilevile kwa sababu ya kukuwa kwa teknolojia wengi ya watu hawa sasa wanahitaji kufanya manunuzi mtandaoni, pamoja na hayo wote tunajua usumbufu unaoweza kuupata ili kupata kadi ya benki yenye kuweza kufanya manununzi mtandaoni, ndio maana kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Mastercard inaleta huduma nzuri sana na rahisi ya kufanya manunuzi mtandaoni ya M Pesa Card.
M Pesa Card hii ni huduma mpya kutoka Vodacom ambayo itakuwezesha kupata kadi yako ambayo utaweza kuitumia kufanya manunuzi mtandaoni kwa haraka bila kuwa na haja ya kwenda benk au mahali popote kujisajili na huduma hiyo.


Sasa kama tayari unajua kuhusu huduma hii basi na uhakika tayari umeshaweza kujiunga, ila kama ufahamu basi unaweza kufuata maelezo haya, Kama unatumia laini ya simu ya Vodacom, unatakiwa kubofya namba za M Pesa ambazo ni *150*00#, baada ya hapo chagua Menu namba 4 ambayo imeandikwa Lipa kwa M-Pesa, baada ya hapo chagua namba 6 ambayo imeandikwa M-Pesa Mastercard baada ya hapo kama hii ni mara yako ya kwanza kutumia huduma hii unatakiwa kuchagua namba 1 ambayo imeandikwa Tengeneza Kadi.
Baada ya kutengeneza kadi utaletewa ujumbe mfupi wa maneno wenye tarehe ya kuisha kwa matumizi ya kadi au Expiry, namba ya utambulisho wa kadi au Card number yenye tarakimu tisa, pamoja na CVV yenye tarakimu tatu. Mambo yote haya ni muhimu sana pale utakapo taka kufanya manunuzi mtandaoni hivyo hakikisha unahifadhi meseji hiyo kwaajili ya matumizi ya haraka.
Sasa kukupa ufafanuzi kidogo ni kuwa, namba hizo zilizopo kwenye meseji hiyo ndio M-Pesa Card, hiyo ni Virtual Card au tuseme kadi ya kidigitali ambayo sio ile ya kushikika ambayo unapewa benki, bali hii ni kadi ambayo unaweza kuitumia bila kuwa na kadi ile ya plastiki, na matumizi yake ni sawa kabisa na kadi ya kawaida yenye uwezo wa kufanya manunuzi mtandaoni.
Kumbuka pale unapotaka kufanya manunuzi unatakiwa kujua namba hizo na hakikisha unaweka pesa kwenye kadi yako kwa kuingia kwenye menu ya M-Pesa kisha chagua 4 kisha chagua 6 alafu chagua namba 3 ambayo imeandikwa weka pesa kwenye kadi, kisha ingiza kiasi kisha subiri kidogo utaletewa meseji yenye kukutaka kudhibitisha kwa kubofya 1 au kubatilisha kwa kubofya 2, baada ya hapo kama umethibitisha utaletewa sehemu ya kuandika password yako ya M-Pesa na baada ya muda kidogo utakuwa umamaliza kuweka hela na utaletewa ujumbe kuwa pesa imewekwa kwenye kadi yako.
Baada ya hapo sasa utaweza kufanya manunuzi mtandaoni kwa urahisi na haraka. Ukweli huduma hii inarahisisha mambo mengi sana kwa watanzania hivyo ni matumaini yangu sasa huduma nyingi zitaweza kulipiwa kutokana na kuwezeshwa kwa huduma hii.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa