Tetesi : Oppo Find X Kuwa Simu ya Kwanza Kuja na RAM GB 10

RAM ni kiungo cha muhimu sana kwenye simu za mkononi, RAM husaidia simu kufanya kazi kwa haraka na pia husaidia simu kuwa na uwezo wa kufungua programu nyingi kwa wakati mmoja, vilevile RAM ni muhimu kwa wale wapenzi wa kucheza Game kwenye simu kwani hii ndio uchukua nafasi kubwa kwa kukupa uwezo wa kucheza game bila kukwama kwama.
Sasa baada ya kujua umuhimu wa RAM kwenye simu sasa hebu ngoja nikujuze hili, hivi karibuni utanza kuona simu zenye uwezo mkubwa wa RAM kama ilivyo kompyuta. Hayo yamebainika baada ya kampuni ya Oppo kuonekana ikitrajia kuleta simu yake mpya yenye uwezo wa RAM ya GB 10.
Kupitia tovuti ya TENAA ambayo hutumiaka kutoa vibali kwaajili ya simu zote zinazoingia sokoni au zinazotarajia kuingia sokoni nchini China, simu hiyo ambayo ni toleo jipya la simu ya Oppo Find X limeonyeshwa kuja na RAM kati ya GB 10.
Mbali na hayo simu hiyo imeonekana kuja na kila kitu kinacho liangana na toleo la kwanza hivyo ni RAM pekee ndio inayotazamiwa kuongezeka kwenye toleo jipya la simu hiyo.
Kwa sasa bado hakua taarifa zaidi kuhusu lini toleo jipya la simu hii litakuja rasmi hivyo kupata habari zaidi kuhusu simu hii hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Swahili Tech.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa