FAHAMU NAMNA YA KUHAMISHA MAFILE KUTOKA KOMPYUTA KWENDA KWENYE SIMU BILA KUTUMIA USB CABLE

As salaam aleikum ndugu msomaji wetu, bila shaka Mara kadhaa tumekuwa tukishindwa kuhamisha mafaili kama picha, video au miziki kutoka katika kompyuta zetu kwenda kwenye smartphones kwa sababu tu ya kukosa USB Cable.


Fikiria umetoka nyumbani na upo ugenini au mgahawani, kuna nyimbo au video moja unayoipenda sana unaiona katika kompyuta ya rafiki yako na unatamani sana uwe nayo kwa muda huo. Ukamuomba rafiki yako akupatie, bila kinyongo akakuruhusu kuichukua, unaanza kuingia kwenye mfuko au mkoba wako kutafuta USB Cable yako ili uweze kuihamisha na unagundua USB uliiacha nyumbani. Unaanza kukosa raha kwa sababu kitu ukipendacho unakikosa kwa sababu ya cable tu.

Ondoa shaka, hapa ndipo ES File Explorer inapoingia. Es File Explorer ni application inayokuwezesha kumanage mafaili yako yote yawe ya katika simu yako, katika kompyuta yako au katika huduma za kuhifadhi data za kimtandao (Cloud Storage).

ES File Explorer ni application ya muhimu zaidi kuwa nayo katika simu yako kama wewe ni mtumiaji wa smartphone. Hebu tuangalie vitu ambavyo ES File Explorer inaweza kukusaidia wewe kama mtumiaji wa Smartphones zinazotumia mfumo endeshi wa Android.

Kuhamisha mafaili kutoka katika kifaa kimoja kwenda kingine kwa kutumia network (mtandao)
Kumanage mafaili ya simu yako yote kwa kutumia Application moja, kama kubadili majina ya mafaili.
Inakuwezesha kucopy na kupaste mafaili mengi kwa wakati mmoja
Inakuwezesha kutafuta (search) faili lolote katika simu yako bila tabu kwa kuandika tu jina la faili
Inakuwezesha kubadilisha muonekano wa mafolder yako, kama kuyapanga katika mpangilio mzuri zaidi.

Inakuwezesha kuyazip mafaili yako (kuyabana na kuyapunguza ukubwa) ili kuweza kuyatuma kwenye barua pepe kirahisi.
Kuangalia video au kusikiliza mziki kutoka kwenye kompyuta yako bila kuzisave kwenye simu yako (streaming)
Kulinda mafaili yako ya muhimu kwa password.

Jinsi ya kuhamisha mafaili kutoka katika kompyuta kwa kutumia ES File Explorer
Pakua (download) ES File Explorer kwenye simu yako kutoka Google Play Store au unaweza ukatumia linki hii ES File Explorer

-Install hiyo Application katika simu yako

-Washa WiFi Hotspot katika simu yako ili kuweza kupata network itakayounganisha simu yako pamoja na kompyuta yako, fanya hivyo kwa kwenda kwenye Settings–>More–>Tethering & portable hotspot–>Wi-Fi hotspot. Washa hapo alafu fungua sehemu hiyo hiyo ili kuset jina na password utakayotumia katika Wi-Fi yako.


-Nenda kwenye kompyuta yako na unganisha Wi-Fi inayorushwa na simu yako kwa kuingiza password ileile uliyoiweka kwenye Wi-Fi hotspot.

-Baada ya kompyuta yako kuunganishwa na Wi-Fi, nenda kwenye folder au File unalotaka kulihamisha, right click na nenda mpaka kwenye Properties, mara nyingi inakuwa chini kabisa.

-Baada ya properties kufunguka, nenda kwenye sharing alafu bonyeza share, everyone ili isikupe shida baadae. Ukimaliza funga hilo file.

-Baada ya hapo nenda kwenye simu yako kisha fungua ES File Explorer

-Bonyeza alama ya menu upande wa kulia juu ya application yako, kisha nenda mpaka kwenye network–>LAN

-Baada ya LAN kufunguka, bonyeza alama kama ya duara hivi kwa juu ili uweze kusearch vifaa vilivyopo karibu na wewe vinavyotumia network moja. subiri kwa muda, ikimaliza utaliona jina la kompyuta yako au ya rafiki yako katika application yako.


-Bonyeza hilo jina ili uweze kuifungua, itakuletea sehemu ya kuingiza username na password ya hiyo kompyuta’ utaingiza username na password za ile kompyuta.

-Baada ya hapo utaweza kuona mafaili yote uliyoyaruhusu kwenye sharing na utaweza kuyahamisha bila tabu kwa kuyabonyeza tu.

Kumbuka: Unaweza ukatumia Wi-Fi ya ofisini, nyumbani au shuleni kuhamisha mafaili bila kutumia Wi-Fi Hotspot ya simu yako. Ila ni vyema kutumia Wi-Fi Hotspot ili kuongeza usalama wa mafaili yako na kasi ya kuhamisha. Sio lazima uwe na kifurushi cha data kufanya hivi.

Tutakuletea makala maalumu  ya ES Explorer ili uweze kuielewa zaidi application hii katika makala zinazokuja, usikose kutembelea tovuti hii ili kuweza kupata maujanja zaidi.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa