Ondoa shaka, unaweza ukarudisha mafile yako yaliyojificha bila tabu na kuendelea na presentation yako. Kitu cha muhimu kufahamu ni kwanini mafile yako yamejificha?
Sababu zinazosababisha kujificha kwa mafile katika USB Flash drive yako
- Virusi vya kompyuta
- Settings za kompyuta yako
- Hitilafu katika Flash
Kuna njia tofauti za kurudisha mafile yaliyofijicha kutegemea na sababu iliyosababisha kujificha kwa mafile hayo
Njia ya Kwanza: Hapa inategemea na toleo la mfumo endeshi unalotumia, kwa watumiaji wa Windows 8, 8.1 na 10 fungua This Pc au My Computer, na angalia katika ribon ya juu ( Menu bar), chagua view–>tiki sehemu iliyoandikwa Hidden Items na hapo mafaili au mafolder yaliyojificha yataonekana.
Njia ya Pili: Hii ni kwale ambao mafile au mafolder yao yamefichwa na virus, hapa tutamia cmd ili kuweza kurudisha mafile yetu yaiyojificha.
Related Article
Fungua Command Prompt kwa kubonyeza alama ya Windows + X kwa pamoja, shusha mpaka kwenye Command Prompt ili kufungua. Au unaweza ukafungua start menu kwa watumiaji wa Windows 7, fungua run alafu andika cmd kisha bonyeza enter ili kufungua.
Hapa tufanye pendrive (flash) yako imepewa herufi G: kwenye windows explorer, alafu andika komandi zifuatazo au Copy na Kupaste komandi hizi kwa right click kwenye cmd na kupaste,
attrib -h -r -s /s /d g:\*.*
Badilisha herufi g: kuwa herufi za flash yako. Alafu bonyeza enter , utaona mstari huo wa maandishi unarukia katika mstari wa pili. Hapo mafile yako yote yaliyojificha yataonekana yote hata kama yalikuwa yamefichwa na virus.
Njia ya Tatu: Tumia Antivirus program unayoiamini kama Kaspersky au Norton kuscan Flash yako au unaweza ukadownload tool itakayokusaidia kuondoa virus aina ya Autorun hapa. http://ccm.net/download/download-11613-autorun-exterminator . Kisha install, hii itakusaidia kuondoa autorun.inf wote waliopo kwenye kompyuta yako pamoja na kwenye flash drive yako.
Zingatio: Hakikisha una install Antivirus Program ya kuaminika katika kompyuta yako au update antivirus iliyopo ili kukuongezea usalama.
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa