TWITTER WABORESHA SEHEMU YA DIRECT MESSAGE [DM]

Mtandao wa Twitter unaendelea kufanya maboresho mapya kila siku, Hivi karibuni Twitter ilifanya mabadiliko ya sheria zake ambapo sasa watumiaji wanapaswa kuwa na akaunti ambazo ziko hai huku umakini zaidi ukihitajika kwa wale wenye akaunti zaidi ya moja.
Mbali na sheria hizo, Twitter hivi karibuni pia imeondoa akaunti feki zaidi ya milioni pamoja na akaunti nyingine zaidi ambazo zinasemekana kuhusishwa na propaganda mbalimbali. Sasa wakati zoezi hilo likiendelea mtandao huo Juzi umetangaza sehemu mpya kabisa ya Quality Filter.
Sehemu hiyo mpya ambayo imetangazwa rasmi juzi, itamruhusu mtumiaji kuweza kuzuia meseji mbalimbali kutoka kwa watu ambao huwajui huku ukiweza kupata meseji kutoka kwa watu unao wafahamu kwa urahisi zaidi.



Kupitia sehemu hiyo ya Quality Filter kutakuwa na sehemu mbili sehemu moja ya Request, na sehemu nyingine ya Inbox. Sehemu ya Request itakuwa inatumika pale mtu usiye mjua atakapo kutumia meseji na sehemu ya Inbox itakuwa inatumika wakati mtu unayemjua atakapo kutumia meseji. Kwa mujibu wa Twitter, sehemu hii itakuwa ikileta urahisi kuunganisha watu kwa kutenganisha meseji kutoka kwa watu unao waju na usio wajua.
Sehemu hii inatagemewa kuja siku za karibuni kwenye app za Android na iOS. Sehemu hiyo itakapo kuja utaweza kuiwasha sehemu hiyo kupitia kwenye sehemu ya DM kwenye app yako ya Twitter kisha bofya kitufe cha Settings ndani ya DM na utaweza kuona sehemu hiyo ambayo itakuwa imeandikwa Quality Filter.
Kwa sasa bado sehemu hii haijawafikia watu wote hivyo hakikisha una update app yako ya Twitter kupitia masoko yote ya Play Store kwa Android na App Store kwa iOS ili kupata sehemu hiyo.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa