JINSI YA KUTAFUTA SIMU ILIYOPOTEA

Android Device Manager itakuwezesha kuiloki simu yako iliyopotea, kuipiga na ikaita kwa nguvu hata kama ilikuwa kwenye silent mode, kufuta data zilizokuwemo pamoja na kuonyesha eneo ilipo kama bado haijazima.

Sio mara zote huwa tunakumbuka sehemu tulipoweka simu zetu na hii huwa inatoa changamoto sana kwetu. Fikiria umeamka asubuhi na umeshajiandaa tayari kwa kwenda kibaruani, unatafuta simu bila mafanikio na muda unazidi kwenda. Hofo ya kuchelewa kazini inaongezeka hasa katika kipindi hichi cha hapa kazi tu na unajikuta umechanganyikiwa kabisa.
Kitu kikubwa tunachofanya katika mazingira kama haya huwa tunajaribu kujipigia labda inaweza ikaita na ukajua ulipoiweka. Sasa je, kama simu yako ilikuwa katika silent mode wakati unalala unadhani utafanyaje?
Hapa ni rahisi tu, watengenezaji wa mfumo wa android waliliwaza hili na kuamua kuleta mfumo maalumu wa kusaidia watu waliopoteza simu zao. Huduma hii inafahamika kama Android Device Manager ambayo itakuwezesha kupiga simu yako na ikaita hata kama ilikuwa kwenye silent mode, kuiloki ukiwa mbali, kufuta data zilizokuwemo kwenye simu yako pamoja na kuonyesha eneo ilipo kama ilikuwa bado haijazimika. 

Njia za kufuata ili kutafuta simu yako iliyopotea;

  • Tembelea Android Device Manager ya Google kwa kutumia kompyuta yako kwa kugonga hapa
  • Ingia kwa kuweka taarifa zako za Gmail kama zile ulizotumia katika simu yako na Google play. Hapa namaanisha Email yako na Password.
  • Baada ya kuingia utaona vitu vinne, Jina la Simu yako na tarehe ya mwisho kuingia, na option (machaguo) nyingine za Ring, Lock na Erase.
  • Ukibonyeza option (chaguo) la Ring simu yako itaita kwa sauti kubwa sana hata kama uliiweka katika silent mode, hii itakusaidia kuipata kiurahisi kama umesahau mahali ulipoiweka.
  • Pia unaweza ukailoki kwa kubonyeza chaguo la Lock, hapa simu utaletewa ukurasa wa kuingiza maneno amabyo utataka yatokee kwenye simu yako, unaweza ukaingiza namba yako ya simu pamoja na maneno kama “Tafadhali irudishe simu kwa mmiliki wake au piga namba hizo”.
  • Kama unahisi simu yako ilikuwa na taarifa za muhimu sana basi chaguo la ERASE ndio mahali pake, hii itafuta kila kitu kilichomo kwenye simu na kuokoa data zako zisianguke mikononi mwa watu.
  • Pia kuna sehemu ya kuonyesha eneo ilipo kwa kutumia ramani kubwa inayoonekana katika kioo cha kompyuta yako kwa wakati huo.
Pia kwa sasa Google wameleta njia rahisi tu ya kutafuta simu yako kwa kuandika Lost Phone katika ukurasa wao wa kutafuta na kama umelogin kwenye akaunti yako google watakuletea ramani ya eneo ilipo simu yako.
Unapoamua kuiloki simu yako kupitia huduma hii tafadhali usisahau Password yako.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa