JAPAN YAANZA RASMI MRADI WA KUTENGENEZA MAGARI YANAYOPAA

Mradi wa kutengeneza magari yenye uwezo wa kupaa umeanza rasmi nchini Japan. Kulingana na vyombo vya habari kampuni 20 zinashirikiana katika kuhakikisha mradi huo unafanikiwa.

Uber, Japan Airlines, Airbus, Boeing, NEC, Toyota, ANA na Yamato ni kati ya kampuni zinazohusika katika kushirikiana utengenezaji wa gari hilo la kipekee. 

Mpango wa gari zinazopaa unatarajia kukamilika ifikapo mwaka 2020. Matumizi ya magari yenye uwezo wa kutumia njia ya anga yatasaidia kupunguza msongamano wa magari barabarani katika miji mikubwa duniani.

Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda nchini Japan imesema kuwa mradi huo utatumia bajeti ya $40.4 milioni kukamilisha mradi huo wa kipekee.

Wajumbe kutoka makampuni hayo watakutana Agosti 29 2018 katika mkutano wao wa kwanza ukifanyika kila mwezi kujadili namna ya kufanikisha mradi huo mapema iwezekanavyo.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa