MFAHAMU CORTANA, MSAIDIZI WAKO WA KWELI NDANI YA WINDOWS 10

As salaam aleikum ndugu yangu Jifunze kila kitu, jifunze kila siku tuendelee na mpya yetu hii Hey Cortana, hii ni komandi ya sauti inayotumika kumwamsha Cortana ili aweze kukusaidia.

Matoleo ya zamani ya windows kama windows XP, windows Vista, windows 7 pamoja na windows 8 kulikuwa na msaidizi mzuri pale ulipokuwa unataka kutafuta baadhi ya vitu katika kompyuta yako au hata mtandaoni. Kikubwa ilikuwa ni kufungua sehemu ya kutafuta na kuandika unachotaka kutafuta, alafu unakaa pembeni kusubiria matokeo.

Teknolojia hiyo imetumika katika matoleo yote ya nyuma ya windows kabla ya windows 10, hali imekuwa tofauti kidogo katika windows 10. Windows 10 imekuja na msaidizi wa sauti anayejulikana kama Cortana. Je, Cortana ni nini hasa?

Cortana ni programu inayokuja na windows 10 inayokusaidia wewe mtumiaji wa kompyuta kutafuta kila kitu unachotaka katika kompyuta yako au mtandao kwa kuipa amri ya sauti tu. Mfano unataka kutafuta programu ya paint katika kompyuta yako, unachotakiwa kufanya ni kufungua programu yako ya cortana, pembeni tu ya Start menu kuna kama duara, huyo ndio Cortana, andika unachotaka kutafuta hapo au bonyeza alama ya kinasa sauti na toa amri yako kwa Cortana.

Kuna vitu vya kuzingatia kabla ya kutumia Cortana. Cha kwanza unatakiwa ufahamu kuwa programu hii kwa sasa inafanya kazi vizuri na lugha ya kiingereza, pili kama kitu hakipo katika kompyuta yako Cortana atajaribu kufungua kivinjari chako na kutafuta matokeo mtandaoni. Tatu, ni vizuri kuruhusu Hey, Cortana feature ili Cortana afanye kazi yake vizuri.

Jinsi ya kuseti Hey, Cortana feature ni rahisi, fungua sehemu ya search hapo pembeni ya start menu, alafu settings, alafu tafuta sehemu iliyoandikwa Note. Utaseti mipangilio kulingana na matakwa yako, baada ya hapo ni wewe na Cortana tu.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa