WAFAHAMU WATU 10 WA KWANZA KUTUMIA MTANDAO WA FACEBOOK

as salaam aleikum ndugu yangu, Je' unawafahamu ni Wakina nani walikuwa watumiaji 10 wa kwanza wa mtandao wa Facebook? Hawa ni wanafunzi wa Havard University walioonyesha mapenzi ya kujaribu mtandao wa bluu kama ulivyokuwa ukifahamika katika siku zake za mwanzoni.

Facebook, mtandao wenye watumiaji takribani bilioni 1.9 kila mwezi na unaoshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani kwa mwaka wa 12 mfululizo. Swali linalotia mzuka ni nani na nani walikuwa watumiaji 10 wa kwanza wa mtandao huu? Ipo wazi kabisa kuwa Mark ndio alikuwa mtumiaji wa kwanza kabisa, ila je wa pili, watatu wanne na watano alikuwa nani.

ID namba za kwanza za mtandao huu hazikuwa zinafuata mlolongo kamili, kama mmiliki na mtumiaji wa kwanza wa mtandao huu Mark Zuckerberg ana ID ya 4.

Haya sasa hawa ndio watumiaji 10 wa kwanza wa mtandao huu

1. Mark Zuckerberg (ID – 4):


CEO huyu lazima alikuwa mtu wa kwanza kuwa na akaunti katika mtandao huu. Mark Zuckerberg alitengeneza mtandao akiwa chuoni Havard na alijipa ID namba 4 kwakuwa tatu za mwanzo alikuwa amezipoteza katika majaribio. Mark ana watoto wawili aliyezaa na mchumba wake wa muda mrefu Priscilla Chan.


2. Chris Hughes (ID – 5):
Huyu ni mtu wa pili katika orodha wa wagunduzi wa mtandao huu akiwa na namba 5 kama ID yake.Ni mhitimu wa chuo cha Havard na alihudumu kama msemaji wa Facebook mpaka mwaka 2007 alipoamua kumuunga mkono Obama katika kampeni zake za Urais.Kwa sasa Hughes ni Mkurugenzi na Mhariri Mkuu wa gazeti la chama cha Republican The New Republic magazine.


3. Dustin Moskovitz (ID – 6):

Bwana Dustin alikuwa room mate (mwanachumba) wa Zuckerber kipindi wapo chuo na ni mmoja ya watu walioanzisha mtandao huu kwa mara ya kwanza. Zuckerberg alimpa Moskovitz kazi ya kuziba mianya ya usalama katika facebook baada ya kusoma PHP kwa muda mfupi tu. Alikuwa makamu wa rais wa wahandisi wa mtandao huo kabla ya kutimua Facebook akiwa na rafiki yake Justin Rosenstein mwaka 2008 na kwenda kutengeneza Asana.


4. Arie Hasit (ID – 7):
Alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwa na akaunti katika mtandao huu japo hakuwa mmoja wa wagunduzi wa mtandao huu. Akiwa Havard alikuwa akisoma shahada ya historia ya mambo ya Israel na baadae alirudi Jerusalem na kufundisha katika chuo kwa kujitolea elimu ya dini na maadili ya Wayahudi.


5. Andrew McCollum (ID – 26):
Huyu ni mmoja wa waanzilishi wa mwanzo kabisa wa mtandao huu aliyekubali kuacha chuo ili afanye kazi na Facebook. Alirudi chuo baadae mwaka 2007 kumalizia shahada ya Kompyuta Sayansi hapo hapo Havard. Kwa sasa ni CEO wa kampuni ya Philo inayojihusisha na usambazi wa Cable Tv katika vyuo nchini Marekani.


6. Colin Kelly (ID – 27):
Huyu ni mtaalamu wa masuala ya Fizikia katika chuo kikuu cha Havard aliyekuwa akijihusisha zaidi na tafiti za kinyuklia chuoni hapo. Baadae alipata shahada ya sheria katika chuo cha Columbia University School of Law, na akajipatia umaarufu sana katika kesi ya kibaguzi iliyohusisha taifa la Marekani na Windsor. Kwa sasa anashi jijini New York.


7. Mark Kaganovich (ID – 28):
Kaganovich alikuwa mtaalamu wa mambo ya kemia na biolojia katika chuo cha Havard na alikutana na Zuckerberg katika darasa la Hesabu, pia walikuwa wakikutana katika mabweni ya chuo hicho. Anakumbuka kipindi bwana Zuckerberg alipokuwa akimlazimisha kuweka profile picture yake kwani alikuwa mzito kidogo kufanya hivyo.


8. Andrei Boros (ID – 29):
Huyu pia alikuwa mtaalamu wa mambo ya Uchumi katika chuo hicho cha Havard. Kwa sasa anafanya kazi katika kampuni ya CapeView Capita huko jijini London.


9. Manuel Antonio Aguilar (ID – 30):

Kwa sasa jamaa huyu ni Rais wa kampuni  inayojihusisha na ujenzi wa nyumba za kuishi za bei nafuu, ya CASSA  (Construcción AutoSuficiente, S.A)


10. Zach Bercu (ID – 31):


Mtaalamu wa mambo ya miale ya kinyuklia anayefundisha katika chuo cha Emory University School of Medicine, alihitimu magna cum laude katika  psychology pale Havard kabla ya kwenda kuongeza elimu katika chuo cha Emory University.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa