JINSI YA KUSOMA UJUMBE WA WHATSAPP KWA SIRI BILA YA ALIYEKUTUMIA KUJUA

As salaam aleikum ndugu Vitiki viwili vya bluu katika Whatsapp vinavyoashiria ujumbe umesomwa vina faida na hasara zake hasa linapokuja suala la kazi au mapenzi.
Kuna muda unajikuta upo busy na mihangaiko ya kimaisha na mmoja kati ya jamaa zako anaamua kukutumia sms Whatsapp, kwa haraka unaiangalia ile sms alafu unaiweka simu mfukoni ukisema nitaisoma baadae. Upande wa mtumaji anapata zile tiki mbili za bluu kuonyesha kama ujumbe wake tayari umesomwa, anakaa kwa hamu kusubiri majibu kutoka wako bila mafanikio. Hapo ndipo chuki zinapoanza kwa kuona kama umedharau ujumbe wake.

Chukulia kama aliyekutumia ujumbe huo ni mama mkwe, au baba mwenye nyumba yako, au bosi wako ama mpenzi wako. Hapo utaona kuna umuhimu wa kuweza kuzima hizi alama za blue zinazoonyesha kusomwa kwa ujumbe.

Tayari tulishaelekezana hapa jinsi ya kuzima last seen, read receipt na kutoa profile picha katika makala iliyopita.

Leo ngoja tuangalie njia ya haraka tu ya kukuwezesha kusoma message za whatsapp bila mtumaji kujua kuwa umeshazisoma.

Pale message ya Whatsapp inapoingia usiifungue kwanza, nenda kwenye settings kisha weka airplane mode on, au bonyeza kitufe cha power moja kwa moja ili kupata menyu ya kuzima data kabisa
Ni muhimu kuzima data au kuweka simu katika airplane mode ili isiwe na uwezo wa kutuma na kupokea data kwa wakati huo. Hii ni kuzuia ujumbe wa kusomwa kwa mesage usirudi kwa mtumaji na kumwonyesha tiki mbili za bluu kwa sababu data ndio inayosafirisha ujumbe huu.
Baada ya hapo fungua application yako ya whatsapp na soma jumbe zako kwa amani.
Ukimaliza kusoma hakikisha unazima application ya Whatsapp kabisa kwa kutumia application manager yoyote uliyokuwa nayo, kisha washa data au zima airplane mode na mtu aliyekutumia atashindwa kuona zile tiki za bluu.
Angalizo: Ni muhimu kuhakikisha unazima data kabisa au unaweka airplane mode ili kuepusha kutumwa kwa ujumbe wa kusomwa kwa message yako. Unapomaliza kusoma hakikisha unaizima kabisa application ya whatsapp.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa