As salaam aleikum Wengi wetu tunatumia huduma za barua pepe bila kujali usalama wa akaunti zetu za barua pepe, tunachojua ni kufungua, kusoma, kutuma na kufuta barua pepe katika akaunti zetu bila kuzingatia usalama na usiri katika akaunti hizo.
Hali imekuwa tofauti sana katika kipindi hichi ambacho taarifa za mtu ni kitu cha muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Katika mataifa yaliyoendelea watu hulipwa pesa nyingi sana kufuatilia taarifa za watu hasa watu maarufu kwa manufaa ya mabosi zao. Mfano mzuri ni kesi nyingi zilizoibuka kati ya mwaka 2013 na 2014 za kimtandao zilikuwa ni za kudukuliwa kwa akaunti za barua pepe za baadhi ya watu mashughuli.
Mashirika ya kijasusi nayo hayapo nyuma katika hili, mfano mzuri ni pale shirika la kijasusi la Marekani CIA walipofanya udukuzi wa simu za Kansela wa Ujerumani na Rais wa Brazil na kuleta tafrani kubwa katika ulingo wa kidiplomasia. Kuna watu hufanya shughuli hii kwa madhumuni ya kibiashara kama kuongeza idadi ya watu wanaotembelea mitandao yao au kujua tabia za mtumiaji na kumpelekea matangazo yanayofanana na kile anachokipenda. Muda mwingine wanatumia njia za udukuaji wa barua pepe ili kufahamu eneo ulipo.
Sasa leo kwa kifupi tunajaribu kukuelekeza jinsi ya kujua kama akaunti ya email ipo salama au kuna watu wanaidukuwa. Wadukuzi wengi wanachokifanya kwa sasa ni kuambatanisha picha au pixels katika barua pepe uliyotumiwa ambazo kiundani zina vijiprogramu vinavyoweza kutuma taarifa zako kwao. Pale unapoifungua tu barua pepe vijiprogramu hivyo vinaanza kufanya kazi yake, swali linakuja je, nitajuaje kama email niliyotumiwa ina vijiprogramu vya udukuzi?
Usiwe na shaka leo nakuletea tool moja inayojulikana kama Ugly Email ambayo itakusaidia katika hilo. Ugly Email itakagua email zako zote zinazoingia kama zimeathiriwa na udukuzi na kukuwekea alama ya jicho katika email zilizodukuliwa hivyo kukusaidia kuzitambua kabla ya kuzifungua. Kwa sasa Ugly email inafanya kazi kwa kutambua email zilizodukuliwa na mashirika kama Yesware, Streak, MailChimp, Mandrill, Bananatag na Postmark japo wanaendelea na kazi ya kuongeza mashirika mengine zaidi ya kidukuzi.
Step 1:
Hizi ni njia rahasi za kufauta ili kutumia Ugly Email:
Step 2:
Fungua kivinjari chako cha google chrome katika kifaa chako
Step 3:
Bonyeza link hii ili kuinstall Ugly Email katika kivinjari chako
Step 4:
Bonyeza “Add to Chrome” katika kivinjari chako na hapo utakuwa umemaliza
Baada ya hapo ukifungua ukurasa wako wa inbox ukiona kuna alama ya jicho katika barua pepe yoyote ujue kuna watu wanaidukuwa.
Je, una maoni yoyote kuhusiana na Makala hii? Tafadhali toa maoni yako hapo chini
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa