GOOGLE INAKUFAHAMU KULIKO UNAVYOFIKIRIA, NI KIASI GANI GOOGLE INAKUJUA SOMA HAPA......

As salaam Aleikum ndugu yangu eti Hujawahi kushangazwa na ile hali ya kila tovuti unayofungua kukuletea matangazo yanayofanana na vitu unavyovipenda au unavyotamani kuwa navyo? Hiyo ni nguvu ya google, inakufuata kila unapoenda kama unatumia moja ya huduma zao.



Google wanatambua mambo mengi unayoyafanya ukiwa online kama tu unamiliki au unatumia moja ya huduma zao, iwe akaunti ya Gmail, Kivinjari cha Chrome, Google Map, Kifaa cha android au huduma nyingine yoyote kutoka Google.

Inawezekana kwa sasa Google wanataarifa za watu wengi zaidi duniani kuliko mtu au kampuni yoyote ile iliyowahi kutokea (japo Facebook wanakuja kwa karibu sana katika hili). Wanafanya yote haya ili kuwafurahisha wateja wao hasa wale wanaotangaza kupitia huduma zao za matangazo.

Ila ushawahi kufikiria nini hasa Google wanafahamu kuhusu wewe? Kwa fikra rahisi tu taarifa zote ulizoziweka kwenye profile yako ya Google+ kama jina, umri, jinsia, vitu unavyopendelea, mazoea yako katika utafutaji vitu google ni vitu vinavyotosha kabisa kuamini kwamba google wanakufahamu.

Taarifa hizi hulingana na vitu gani umeamua google wavitambue au la, kujua ni kwa jinsi gani google wanakutambua jaribu kufanya yafuatayo;

Fungua ukurasa wa akaunti yako ya google (Your Google account page), fanya hivyo kwa kutumia kivinjari chako na weka link hii ile kwenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa akaunti yako. http://myaccount.google.com/

Hakikisha unaingiza taarifa zako kama username na password ili uweze kulogin kwenye akaunti yako, fanya hivyo kwa kubonyeza kiduara cha upande wa kulia kama bado hujalog in.

Watu wengi hawafahamu kama wana akaunti za google, ipo hivi kama unatumia moja ya huduma za google kama Gmail, Drive, Hangout, Android au Calender basi unayo akaunti ya google.

Kuangalia vifaa ulivyowahi kutumia katika kuingia katika akaunti yako ya google

Bonyeza “Sign-in & security” na shuka chini mpaka kwenye “Device activity & notifications”, hapo utaona orodha ya vifaa ulivyowahi kutumia kuingilia katika akaunti yako ya google.


Kama kuna kifaa ambacho hukitumii tena, kibonyeze alafu bonyeza remove ili kukiondoa kwenye orodha. Kama una kifaa kimeibiwa au kimepotea unaweza ukabonyeza find my device on google device manager .

Kuangalia application zinazohusiana na akaunti yako ya google

Kuangalia application gani zinahusiana moja kwa moja na akaunti yako, bonyeza “Connected apps & sites” alafu shusha chini mpaka kwenye “Manage apps”. Chagua zile zile ambazo huzitumii tena alafu bonyeza Remove all.


Sehemu hii inaweza kutumika kuangalia passwords kutoka kwenye Chrome na Android ulizozisave kwa kutumia Google Smart Lock, na kufuta zile amabazo huzitumii tena.

Kuangalia vitu gani umesearch zaidi katika Google, Video unazoangalia zaidi Youtube pamoja na vingine vingi kuhusiana na matumizi yako

Hapa unaweza ukaangalia vitu gani umevitafuta zaidi katika mtandao wa google kwa kubonyeza “Personal info & privacy”.


Katika panel hii unaweza ukaangalia vitu vyote vilivyotajwa hapo juu kwa kushusha chini (scroll down).

Kuangalia maeneo gani unayopendelea kutembelea

Ili kuleta msisimko katika utumiaji, application nyingi zimekuwa zikihifadhi maeneo unayopenda kutembelea, hii inachangia sana kuwafanya google kufahamu maeneo mengi unayopenda kutembelea ukiwa na simu yako yenye akaunti ya google au application inayotumia google.

Ukiw bado kwenye “Personal info & privacy”, fungua kwenye “Places you go” alafu bonyeza “Manage activity,” kuona maeneo yote unayopenda kutembelea.


Hapa itakuletea ramani na kukuonyesha maeneo yote uliyotembelea ukiwa na simu au kifaa chako cha android huku ikiweka alama nyekundu kwa maeneo unayotembelea zaidi.

Ikibonyeza kialama chekundu, itakuonyesha njia uliyopita ili kufika hapo, picha ulizopiga wakati wa safari yako pamoja na maeneo uliyopunzika katika safari hiyo.

Bonyeza alama ya dustbinili kufuta kumbukumbu zote hizo kama huzihitaji. Pia unaweza ukawazuia google wasihifadhi taarifa zako za sehemu unazotembelea kwa kuzima ile batani ya blue mwanzoni kabisa.

Sasa unataka kujua Google wanafikiria nini kuhusu wewe?

Kujua google wanafikiria nini kuhusu wewe jaribu kuangalia taarifa gani wanatumia ili kukuwekea matangazo yanayofanana na vitu unavyovipenda.




Kujua nenda kwenye “Personal info & privacy”, alafu shuka chini mpaka kwenye Ads settings  alafu bonyeza Manage Ads Settings.

Unaweza ukaangalia kama google wanajua umri wako pamoja na jinsia yako hapo, Pia unaweza ukarekebisha baadhi ya taarifa zako katika sehumu hiyohiyo.


Unaweza ukapakua data zako zote hizo kwa ajili ya matumizi yako binafsi kwa kushuka chini kabisa “Control your content”–>“Download your data” –>“Create archive”. Hapo itakupeleka kwenye ukurasa ambao utakuwezesha kuchagua vitu unavyotaka kusave.

Sasa nadhani umeamini Google wana taarifa zako nyingi kuliko hata wewe unavyokumbuka, jaribu kupitia kila taarifa katika ukurasa huo ili kuona ni jinsi gani Google wanakufahamu na kuchagua nini google wahifadhi na nini wasihifadhi.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa