FAHAMU TRICKS 5 MUHIMU KUZIJUA KATIKA WHATSAPP

Nadhani jina Whatsapp sio geni katika masikio ya watumiaji wa simu za kileo (smartphones), hasa kwa wapenda kuchat hapa ndio mahali kwao. Ila ngoja tuangalie baadhi ya vitu tunavyoweza kufanya kwa kutumia application hii kutoka kampuni ya Facebook.

Ikiwa na watumiaji zaidi ya bilioni moja duniani kote Whatsapp ni huduma pekee ya rahisi na haraka ya kuchat kwa sasa ulimwenguni, kuanzia huduma zake za kutuma picha, ujumbe mfupi, kupiga simu pamoja na kutuma video kumeifanya application hii kuwa na watumiaji wengi zaidi. Pamoja na huduma zake zote application hii kwa sasa ni ya bure kabisa tofauti na hapo mwanzo ambapo walikuwa wanatoa miezi 12 ya bure na kuchangia kiasi cha dola 1 ya kimarekani muda huo unapoisha.

Ukiacha kutuma na kupokea ujumbe wa maneno, picha, video au sauti application hii ina huduma nyingi ambazo zinamrahisishia kazi mtumiaji wake. Hebu tuangalie jinsi ya kutumia application hii kwa kufundishana utundu kidogo sababu mara nyingi watengenezaji wa application huwa wanaongeza vitu bila kutangaza.

1. Zima “Read Receipts” (tiki mbili za blue zinazoonyesha ujumbe umesomwa).
Whatsapp walileta huduma hii mwaka jana ya kuonyesha alama ya tiki mbili za rangi ya blue kama ujumbe uliotuma umesomwa (hapo awali tiki mbili za kijivu kuonyesha kama ujumbe umefika), hii inaleta changamoto sana kwa baadhi ya watu na ina faida kwa baadhi ya watu.Fikiria upo kazini na bosi wako, ghafla ujumbe unaingia kutoka kwa mpenzi wako na unaamua kuusoma kwa kuibia ili usionekane na mwajiri wako, unasoma bila kupata nafasi ya kujibu. upande wa pili mpenzi wako anajua kuwa umesoma ujumbe wake ila umegoma kujibu. Hapo kuna haja ya kuwa na njia ya kuzima ili mtumaji asijue kama umesoma ujumbe wake. Whatsapp waliliona hilo hivyo wakaamua kuweka sehemu ya kuzima alama hizi zisibadilike rangi hata kama umesoma ujumbe uliotumiwa.

Fungua application yako ya whatsapp, fungua sehemu ya menu (hapa inategemea na aina ya simu).
Fungua settings–>Accounts–>Privacy–>hapo utaangalia kwa chini kwa watumiaji wa android utaona sehemu imeandikwa Read Receipts na kuna alama ya tiki kwa mbele, cha kufanya gusa hapo kwenye tiki ili kuzima huduma hiyo.
Kumbuka, ukizima read receipts na wewe hutoweza kujua kama message unazotuma kama zimesomwa (Itazima uwezo wa kujua kama jumbe ulizotuma zimesomwa kwa mtu uliyemtumia).


2. Angalia muda gani ujumbe uliotuma umesomwa
Hii ipo tofauti kidogo na zile tick za blue, njia hii inakuonyesha ni muda gani haswa ujumbe wako ulisomwa na uliyemtumia hata kama alizima Read Receipt (zile tiki mbili za blue)

Ni rahisi tu, fungua sehemu ya chat, tafuta ujumbe unaotaka kujua muda uliofika na muda uliosomwa na mtu uliyemtumia. Bonyeza katika ujumbe huo kwa muda (click and hold) wa sekunde kadhaa na kibox kipya kitafunguka kwa juu (pop up), chagua info na hapo utapata taarifa zote za ujumbe wako. Hiyo ni kwa watumiaji wa android, kwa watumiaji wa iPhone fungua sehemu ya chat na chagua ujumbe, alafu futa kuelekea kushoto (swipe left) ili kupata menu mpya itakayokuonyesha sehemu ya info.


3. Ficha Profile Picha, Last seen na Status
Kuna muda mtu unataka uwe na usiri kidogo, fikiria rafiki zako wamekuunga katika group kubwa la whatsapp lenye watu wengi usiowafahamu na hutaki kila mtu kwenye group au mwenye namba zako ajue muda gani upo hewani, aone picha yako na status uliyoweka katika akaunti yako. Ni rahisi tu, hii ni njia nzuri zaidi ya kucontrol nani anaona taarifa zako za whatsapp.

Fungua sehemu ya option upande wa kulia juu ya application yako ya whatsapp, chagua settings–> Account–> Privacy –> alafu nenda kwenye kipengere unachotaka kukidhibiti. kwa mfano last seen unaweza ukachagua visibility iwe ‘Everyone’ Kila mmoja, ‘My contacts’ contacts zangu tu au ‘No body’ kulingana na matakwa yako.


4. Hifadhi baadhi ya message za muhimu ili uzisome baadae (Starred Messages)
Kuna muda unatumiwa message ya muhimu wakati ukiendelea kuchat na mwenzio au wenzio katika group na usingependa kuipoteza hiyo message katika msitu wa messages katika chat, hapo ndipo umuhimu wa starred messages unapokuja, hii itakusaidia kuweza kusoma message zote ulizoamua kuzipa nyota baadae tena kwa urahisi zaidi bila kupekua sana.

Bonyeza kwa muda katika message unayotaka kuipa nyota (star), alafu angalia sehemu ya juu ya chumba cha kuchati ndani ya application ya whatsapp utaona alama ya nyota, bonyeza hiyo alama ya nyota ili kuihifadhi hiyo message. Muda muafaka wa kusoma hiyo message ukifika, fungua option (sehemu ya kulia inakuwa na vidoti vitatu)  alafu chagua ‘starred messages’, hapo utaweza kuona messages zote ulizozihifadhi.



5. Tuma ujumbe mmoja kwa watu wengi bila wao kufahamu
Kuna muda unataka kutuma ujumbe mmoja kwa watu tofauti bila wao kujua kama wmetumiwa ujumbe mmoja, mfano mzuri ni pale unapotaka kuwakutanisha watu waliogombana bila wao kujijua. Nirahisi, tumia huduma ya ‘Broadcast’ katika whatsapp. Chagua watu unaowataka kuwatumia hiyo message, kisha andika message yako kisha itume kwa kutumia broadcast.

Kama una maswali tafadhali toa maoni yako katika sehemu ya maoni hapo chini.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa