JE' UNADHANI HILI NDIO TOLEO LA MWISHO LA SAMSUNG S?

As salaam aleikum, Zikiwa zimebaki siku chache kuzinduliwa kwa simu za Samsung Galaxy S9 na Samsung Galaxy S9 Plus inaelezwa huenda zikawa ndio toleo la mwisho la simu za familia ya S.

Kwa mujibu wa wachambuzi na watafiti wanaofatilia kwa karibu masuala ya simu janja wanasema hatua hiyo itakuja kwa ajili ya kupunguza urefu wa jina wa kuitwa S10 na badala yake toleo lijalo likaitwa “SX”. X itasimama kama namba 10 ni kama vile walivyofanya kampuni ya Apple kwa toleo lake la iPhone X.

Na kwamba inaelezwa matoleo yatakayofatia yatajulikana na kutofautishwa kwa mwaka wa simu ilivyotolewa. Yaani itakuwa Galaxy X (2020), Galaxy XI (2021) na kuendelea lakini hili wachambuzi wa masuala ya simu janja wameliona kutowezekana kwa Samsung kufanya hivyo kwani itakuwa ngumu kutofautisha baina ya toleo moja kwa jingine.
Hata hivyo, vyanzo vinasema Galaxy X itakuwa ni mwisho wa familia ya S na hilo pia litajiri kwa familia ya matoleo ya Note ambayo pia inakaribia toleo Note 9 kutoka mwaka huu. Simu mpya ya Samsung inayotarajiwa kutoka kati ya mwaka 2019 yenye uwezo wa kukunjwa na kujikunjua pamoja na kuwa na vioo viwili inaelezwa itakuwa na jina la Samsung Galaxy X.  Kujua undani wa simu ya Samsung itakayokuwa na vioo viwili BOFYA HAPA.


Hakuna uhakika kama simu hiyo ndio itahitimisha matoleo ya S au la!. Mvuto wa jina na urahisi wake pia huchangia kwa bidhaa kufahamika kirahisi kwa wateja na kununulika kwa wingi. Endelea kutembelea SwahiliTech.net, tutakujulisha mara moja kama kutakuwa na mabadiliko…

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa