HII NDIO SAMSUNG J2 (2017) SIFA NA BEI YAKE


Samsung Galaxy J2 (2017) ni smartphone kwa watu ambao wanataka simu yenye ubora lakini hawana fedha ya kutosha. Ina ubunifu wa kuvutia na inakuja na quad-core Exynos processor pia ina uwezo wa LTE.

Sifa kamili za Samsung Galaxy J2 (2017) ni kama ifuatavyo:

  • 4.7-inch Super AMOLED Display, 540 x 960 pixels (234 ppi)
  • Prosesa: 1.3GHz quad-core Exynos 3475 Quad CPU,
  • Mfumo Endeshi: Android 7.0 (Nougat)
  • Uhifadhi: 1GB RAM, Ujazo wa ndani (Storage) – 8GB na Eneo la memori kadi (External Storage) unaweza kuweka mpaka memori ya ukubwa wa 256GB.
  • Kamera: Kamera ya nyuma (Rear) 5MP na Kamera ya mbele (Selfie) 2MP
  • 4G LTE Data
  • Betri: ujazo wa 2000 mAh

Muundo na Kioo


Related Article

Samsung Galaxy J2 (2017) jinsi ilivyo ni simu yenye muonekano mzuri na muundo safi. Unene wake ni 8.4 millimetres, unatosha ukilinganisha na bei yake. Samsung Galaxy J2 (2017) ina uzito wa kama gramu 130.
Skrini ina ukubwa wa inchi 4.7 na inatumia teknolojia ya Super AMOLED. Japo kuwa screen resolution yake ni 540 x 960 pixels tu, bado unaweza kupiga picha zenye ubora na rangi nzuri.

Kamera na Uhifadhi


Huyu si bingwa wa kupiga picha. Lakini Samsung Galaxy J2 (2017) bado inaweza kutoa picha ambazo unaweza kuzitumia sehemu yeyote. Ina kamera ya nyuma (Rear) ya 5MP na Kamera ya mbele (Selfie) ya 2MP. Samsung Galaxy J2 (2017) ina uwezo wa kuchukua video za HD (720p).
Unapata hifadhi ya ndani (storage) ya GB 8 ila unaweza kuweka mpaka memori ya ukubwa wa 128 GB.

Utendaji na OS

Samsung imetoa simu hii na prosesa yake ya Exynos. Upeo wa kasi ni 1.3 GHz na chip hupata msaada kutoka kwenye RAM ya 1GB. Mpangilio huu unatoa utendaji wa kufurahisha, ikiwa hujafungua programu nyingi kwa wakati mmoja. Samsung Galaxy J2 (2017) inatumia mfumo endeshi wa Android 7.0 Nougat.

Sifa Zingine

Ikiwa unataka kufurahia kasi ya mtandao wa haraka, Samsung Galaxy J2 (2017) itakuwezesha na teknolojia yake ya mawasiliano ya 4G LTE. Unapata betri yenye ujazo wa 2,000mAh. Hii betri inakaa hadi masaa tisa kwenye mtandao wa LTE, kwa mujibu wa Samsung.
Samsung Galaxy J2 (2017) inatoa njia zingine za kuunganisha, ikiwa ni pamoja na microUSB 2.0, Bluetooth 4.1 na Wi-Fi. Kuna GPS na GLONASS kwa mahitaji yako.

Bei na upatikanaji

Samsung Galaxy J2 (2017) haipatikani rasmi nchini Tanzania, Kenya, na Ghana. Hata hivyo, unaweza kuwa na uwezo wa kununua simu ya Android katika maduka ya mtandaoni hapa nchini. Bei ya Samsung Galaxy J2 (2017) inatarajiwa kuanzia shilingi 200,000 hadi shilingi 300,000 kulingana na eneo lako nchini.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa