- Kuna tovuti aina ngapi zinazoweza kukulipa?
Tovuti yoyote ile inaweza kukuingiazia kipato ni kutokana na malengo yako.Naweza kuzigawa tovuti zinazoweza kukuingizia kipato katika sehemu mbili,
- Tovuti inayofunguliwa ikiambatana na biashara uliyo nayo(mfano una kampuni/duka hapo ndio unalifungulia tovuti)
- Tovuti inayofunguliwa isiyoambatana na biashara(hauna kampuni/duka) kama hii swahilitech.net
Hapa nitazungumzia aina ya pili hapo juu(ambayo hauna duka/kampuni).Ili uweze kupata kipato katika aina hii ya pili ya tovuti itakubidi uzingatie masuala yafuatayo;
- Tovuti yako lazima ikidhi mahitaji ya watu(yakiwa mahitaji ya lazima ni vizuri zaidi)
- Iwe na muonekano mzuri
- Iweze kufunguka haraka
- Iendane na hadhira unayokusudia
- Iweze kuonekana vizuri katika simu za mkononi/zenye screen ndogo
- Tovuti ijitangaze yenyewe
- Tovuti uitangaze katika mitandao ya kijamii bure au hata kwa kulipia
- Tovuti uifanyie SEO
- Lazima uisimamie mwenyewe
- Pata ushauri pindi inapohitajika
- Fanya market/keywords research kwa bidhaa/huduma unayotoa.
Muda unatofautiana kutokana na vitu hivi;
1.Aina ya tovuti
2.Mtaji uliotumika/investment
Hapa nitazungumzia aina ya tovuti. Tovuti zinazofunguliwa kutoa huduma fulani ambayo ni muhimu na lazima hizi zitachukua muda mfupi kuanza kukulipa,ukilinganisha na tovuti zitazofunguliwa kutoa huduma ambazo sio za lazima. Mfano umefungua tovuti ya kuuza bidhaa hii inaweza kuanza kukulipa ndani ya mwezi mmoja toka uifungue,Kwa hiyo muda wa kuanza kukulipa inatokana na muda wako katika tovuti hiyo.Usipoifanyia online/offline promotion haiwezi kukulipa kabisa.
kila kitu ni juhudi ili uweze kufanikiwa katika jambo hilo ni lazima ujitolee kwa hali na mali.
matumaini yangu umepata mwanga japo kidogo kuhusu makala yetu hii sambaza na marafiki wengine wajue jambo hili.
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa