HII NDIO TECNO PHANTOM 8, BEI NA SIFA ZAKE

Tecno ni kampuni kubwa nchini Tanzania tangu ilipoanza kuuza simu zake. Kampuni hiyo ni miongoni mwa kampuni za kwanza kuanzisha vifaa vya SIM-mbili (dual-SIM) ili kuwavutia watu ambao wanataka kutumia zaidi ya mtandao mmoja wa simu za mkononi. Kwa jitihada zake za kushindana na kuingia katika soko ambalo lilikuwa limetawaliwa na simu janja, Tecno ilianza kutoa smartphone mwaka 2012, na ni sahihi kusema kuwa vifaa vyake vilipokelewa vizuri, hasa barani Afrika na Kusini mwa Asia ambapo sasa inafanya kazi.
Uzinduzi wa juzi kati, ambao umehitimishwa huko Dubai, umeonyesha kuanzishwa kwa kifaa chake, Phantom 8. Kwa hiyo, Phantom inaleta nini juu ya meza katika uwanja wa smartphone wenye upinzani mkubwa, na hasa nchini Tanzania ambapo OEMs pinzani kama vile Samsung na HMD Global wameboresha vifaa vyao (Galaxy Note 8 na Nokia 8) ? Mengi, kwa kweli, hebu tuiangalie kiundani.
Phantom 8 imefanya vizuri kwenye upande wa kamera, ambapo, bila shaka, ni kipengele muhimu cha mnunuzi yeyote wa simu. Ina kamera mbili Sony IMP386 12 MP na sensor 13 MP. Ya kwanza ina uwezo wa kuzoom wa 2X, huku ya pili ikiwa na 10X Super Zoom ambayo inaongeza hesabu ya megapixel ya picha zinazopigwa ili kutoa shots kali zaidi. Ni kipengele kilichoanzishwa na smartphones ya Apple iPhone 7 ya mwaka jana, na tangu hapo makampuni mengine yameiga teknolojia hiyo, na kila mtengenezaji anaipa jina la kipekee. Samsung wanaiita “Live Focus”, kwa kesi ya toleo la Tecno inajulikana kama Auto Refocus.
Kamera ya mbele ina uwezo wa 20 MP na  ina ‘‘smart dual selfie’’ flash. Kamera ya selfie ni bora zaidi kuliko matoleo ya tecno yaliyopita, na inajumuisha vipengele kama vile “Smooth Mode” na “Brighten Mode”.
Simu hii ina RAM ya 6GB . Vipengele vingine vinajumuisha uunganisho wa kimataifa na 4G + ambayo ina uwezo wa 300 Mbps kwenye downloads, inawezeshwa na Android 7.0 Nougat, ambalo sio toleo jipya zaidi la Android, inasikitisha.
Phantom 8 ina kioo cha 5.7-inch na resolution ya 1080 * 1920. Pia kuna “Type-C port” kwajili ya kuchaji na kufanya uhamisho wa data . Betri yake ya 3500mAh inaweza kujazwa hadi 100% ndani ya dakika 70, hii imeshangaza wengi.
Huenda umegundua kwamba kifaa hiki kinaweka msisitizo juu ya uwezo wake wa kamera, ambayo tutaijaribu mara tu tutakapo ipata na kuifanyia uchambuzi, hivi karibuni. Jambo lingine ni kwamba hakuna matoleo mawili ya kifaa hiki kama tulivyooona mwaka jana ujio wa Phantom 6 na Phantom 6 Plus. Hii ni mbinu inayokubalika kwa maoni yangu kwa maana ina maana kampuni itahitaji tu kuzingatia kifaa kimoja kutoa msaada wa kiufundi.
Tecno Phantom 8 itakuwa inapatikana katika rangi 3; Galaxy Blue, Phantom Black na Gold Champagne. Itakuwa na gharama karibu na TSH 865,596.00 (inaweza kubadilika) itakapo zinduliwa nchini Tanzania katika siku zijazo. Ni bei ya ushindani kwa sababu haizidi vifaa mbalimbali vya gharama nafuu.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa