FAHAMU MAMBO HAYA MUHIMU YAKUZINGATIA KABLA UJATENGENEZA APP YA ANDROID

As salaam aleykum, Android ni mfumo (operating system) ambao ni maarafu sana kwa kuwa umefanikiwa kutumiwa kwenye vyombo vya kielectroniki kama simu, saa, tv, laptops, tablet na hata kwenye magari ya kisasa pia utakuta android.
Hii ina maanisha kama wewe una ndoto za kuwa android developer basi hujakosea kufanya maamuzi maana android ni mfumo ambao unatumiwa ulimwenguni kote na una endelea kukua kwa kasi kubwa na kutapakaa kwenye vitu vingi vya kielectroniki.
Ili kuweza kutengeneza Android app basi unapaswa kujua Java pamoja na XML(Extensible Markup Language). Wengi wetu tukishasikia tu Java basi tunakata tamaa. Lakini hutakiwi kuogopa maana Google wanajaribu kila siku kurahisisha utengenezaji wa android app.
Pia Google wana website inayo toa mafunzo jinsi ya kutengeneza android app pamoja na mifano mingi ambayo itakusaidia wewe kuweza kutengeneza app yako. Unaweza tembelea hiyo website kwa kutumia link chini
https://developer.android.com/index.html
Leo tutaangalia mambo yanayoitajika ili kuweza kutengeneza android apps.

Computer

Ili uweze kutengeneza android app unaitaji computer ambayo ina uwezo au sifa zifuatazo.

Kama una computer ya windows basi hakikisha computer yako ina sifa kama za hapo juu. Pia kama una Mac na linux basi hakikisha ina kidhi vigezo vyote kama hivyo hapo juu.

Android Studio


Android Studio ndio program inayotumia kama IDE (integrated development environment). Inamaanisha kwamba shughuli nzima ya kutengeneza android app, kuijaribu na hata kuiweka kwenye playstore itafanyikia kwenye android studio. Pia shughuli zote za ku test app yako zinafanyika ndani ya android studio.
Kwa kutumia android studio utaweza kutengeneza apps za simu, saa, android auto pamoja na android Tv. Android Studio imetengenezwa na Google ili kurahisisha shughuli za ku design android app. Unaweza download android studio kwa kutumia link chini kisha install kwenye computer yako
https://developer.android.com/studio/index.html

JavaSe (Java Development Kit)


programming language ambayo inatumika kutengeneza Android app ni Oracle’s Java SE. Java SE ilitengenezwa na Sun Microsystems na baadae ikanunuliwa na Oracle.
Zipo aina tatu za Java. Kuna Java EE (Java Enterprise Edition) ambayo hii hutumika kwenye network ya macomputer makubwa. Halafu kuna Java ME (Java Micro Edition) ambayo utumika kutengeneza mobile application. Java SE ina uwezo mkubwa kuliko Java ME na ndio inatumiwa na Google kutengeneza Android Os.
Ili kuweza kuweka JavaSe (Java Development Kit) kwenye computer yako unatakiwa kutembelea link chini kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa download. Hakikisha ume download na ku-install JavaSe (Java Development Kit) maana bila kufanya hivyo hutaweza kutengeneza android app.
http://www.oracle.com/technetwork/java/javase/downloads/index.html
Hivyo vitatu ndivyo vitu vya muhimu ambavyo una hitaji ili uweze kutengeza android applications.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa