1. Chapisha tangazo katika blog yako ya zamani
Hii ni njia moja wapo ya kuwaarifu watembeleaji wa blog yako, kuhusu blog yako mpya chapisha tangazo katika post yako ya mwisho, au unaweza kuweka banner juu au chini ya menu kuhusu blog yako mpya, utaweza kuwasaidia watembeleaji wako kufahamu kuhusu mabadiliko ya blog yako bila shida.
2. Tumia mitando ya kijamii
Kama unawafuatiliaji wengi katika mitandao yako ya kijamii kama Facebook, Twitter, Google+ n.k, hii itakupatia urahisi wa kuwajuza watembeleaji wako kuhusu blog yako mpya, hivyo wafahamishe wafuatiliaji wako katika mitandao ya kijamii kuhusu blog yako mpya hii itasaidia kwa kiasi kikubwa.
4. REDIRECT blog yako ya zamani kwenda katika blog mpya
Unaweza kuwaelekeza watembeleaji wako wa blog ya zamani kwenda katika blog yako mpya kwa urahisi mno kwa kuweka code nitakazo kupa hapa chini na kwa kuziweka katika template ya blog yako ya zamani. baada ya kuweka code hizi watembeleaji wako wataelekezwa automatic kwa kutembelea blog yako ya zamani baada ya sekunde chache wataamishwa na kuletwa katika blog yako mpya. fuata hatua hizi hapa chini ili zoezi hilo litimie
- Kwanza kabisa ingia/log in katika blogger akaunti.
- kisha bonyeza “Template” . kama inavyoonekana pichani hapa chini:
- Baada ya hapo, bonyeza “Edit Html”. kama inavyoonekana pichani hapa chini
- Kisha angalia code hii <head> katika template kama inavyoonekana pichani hapa chini:
- Kisha chini ya code <head>, Paste code hizi kwenye kisanduku hapa chini:
1
|
<span style="color: red;"><b><meta http-equiv="refresh" content="0;url=http://www.riyadibhai.blogspot.com/"></meta></b></span>
|
- badilisha link www.riyadibhai.blogspot.com weka link yako tayari umefanikiwa , bonyeza “Save Changes” furahia sasa.
Maneno ya muandishi
kipindi hiki nimekuwa busy mno, nimebanwa na majukumu ya kujitafutia riziki hivyo nakosa muda mwingi wa kuwaletea mambo mengi hivyo itabidi turidhike na hiki kodogo, kumbuka mimi ni binadamu na nakosea pia kama kuna makosa ya kiandishi au yeyote kuhusu makala hii basi usisite kuniachia mani yako hapo kwenye sanduku la maoni, maoni yote ninayapenda ila usitumie lugha chafu karibuni.
Imeandikwa na Riyadi Bhai
Riyadibhai.blogspot.com | Sambaza kama ilivyo
Vyanzo
Picha ya kwanza kutoka mtandaoni
code kwa msaada wa ndugu yangu Ravi kumar
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa