TUJIKUMBUSHE : PICHA 5 TULIPOTOKA NA TULIVYOSASA KATIKA ULIMWENGU WA TECHNOLOGY

Hebu leo tukumbuke tulipotokea katika vizazi tofauti vya teknolojia kuanzia kutumia redio za kaseti, Santuri mpaka CD, kutoka kutumia nokia jeneza mpaka leo Galaxy S7 Kutumia tv ya chogo mpaka flat screen.

Simu hizi za mezani zilijizolea umaarufu mkubwa sana katika kipindi cha miaka ya 80′ na 70′ duniani. Zikiwa zinatumia waya katika kuonganisha pointi moja na nyingine zilikuwa msaada mkubwa sana kwa kipindi hicho. Ofisi za serikali na baadhi ya mashirika ndio walikuwa na uwezo wa kuwa nazo.
Televisheni za kutune kwa kipindi hicho zilikuwa katika ubora wake, kwa nchini kwetu Tanzania watu wawili wa kwanza kumiliki Televisheni kwa mujibu wa chanzo kimoja walikuwa ni Baba wa Taifa na Sheikh Yahya japo haina uhakika sana kama walikuwa wanatumia aina hii ya Tv. Kituo pekee cha TV kilikuwa kituo cha Televisheni cha Zanzibar.
Simu za mkononi za kwanza kutumika nchini zilikuwa kubwa kama zinavyoonekana katika picha nyingi zikiwa kutoka kampuni ya Siemens na Motorola. Huku kukiwa na mtandao mmoja mkubwa wa simu wa Mobitel katika baadhi ya maeneo ya mijini.
Santuri ni jina geni kwa vijana wengi wa kizazi cha sasa, ikiwa na uwezo wa kuwekwa nyimbo mpaka za dakika 45 santuri ndio ilikuwa njia pekee ya kusikiliza muziki maridhawa katika baadhi ya klabu nchini.
Redio za Cassette za kutembea nazo maarufu kama Walkman kwa kipindi hicho zilikuwa zinabamba sana, kutoka kwenye walkman teknolojia ikatupeleka katika mp3, iPod na mpaka sasa hakuna haja ya kuwa na vifaa hivi kwa sababu 100% ya kazi zake zinafanywa na simu.
Kama unakumbuka zaidi unaweza ukashare nami katika sehemu ya maoni hapo chini.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa