JINSI YA KUPAKUA (DOWNLOAD) VIDEO YOUTUBE KWA KUTUMIA TUBEMATE

Moja ya kitu tunachokifurahia zaidi katika simu zetu (smartphones), ni uwezo wa kuangalia video za Youtube moja kwa moja. Lakini kuna kikwazo katika hili, ili uweze kuangalia video kutoka Youtube ni lazima uwe na kifurushi cha data cha kutosha, hapa ndipo umuhimu wa kujua jinsi ya kudownload video hizi unapokuja.

Hali sasa imekuwa tofauti hapa nchini kwetu linapokuja suala la vifurushi kutoka katika makampuni ya simu, unapotaka kujiunga lazima uchague ni aina gani ya kifurushi unahitaji ili kukidhi mahitaji yako. Tofauti na hapo awali, kifurushi kimoja kilikuwa na dakika, sms na data za kutosha kuperuzi siku nzima. Hivi sasa ni lazima uchague kununua kifurushi cha data au cha dakika za maongezi na sms ili kuweza kutimiza mahitaji yako. Hakuna mtandao wenye afadhali sababu wote wanalingana katika hili, na hii ni kutokana na agizo la mamlaka ya mawasiliano nchini kutaka mitandao yote inayotoa huduma za simu nchini kuwa na vifurushi vinavyofanana.
Asilimia 80% ya video zote tunazoangalia katika simu zetu chanzo chake ni Youtube, nani anayemiliki smartphone na hajawahi kabisa kutumia Youtube (wapo lakini sio wengi wale wanaotumia simu kwa kupiga na kupoke tu).
Kuna muda unatamani video uliyoangalia ibaki katika simu yako ili uweze kuiangalia baadae au kumtumia rafiki yako kupitia whatsapp. Hapa ndipo mtihani unapokuja kwani kwa sera za Google hawaruhusu mtu kupakua (kudownload) video kutoka Youtube hivyo hakuna kitufe au link yoyote itakayokuwezesha kupakua video moja kwa moja.
Kwa msaada wa plugins na application hili linawezekana sasa, leo tutaangalia baadhi ya njia rahisi za kudownload video kutoka youtube,

Njia za kufuata;

Step 1: Download Tubemate kutoka katika tovuti yao
Tubemate ni application ya bure inayokuwezesha kupakua video kutoka Youtube kiurahisi zaidi na katika formats tofauti tofauti. Fungua kivinjari chako (web browser) na bonyeza hapa ili kuweza kupakua application hii kutoka katika tovuti yao. ni vizuri kupakua application hii kutoka katika tovuti yao kwa sababu kuna application nyingi feki zinazotumia jina hili katika playstore. Kuwa makini kuchagua link ya Android Freeware kama utaamua kwenda moja kwa moja kwenye website yao kwa kutumia adress ya tubemate.net.
Step 2: Inapoanza tu kudownlod simu yako itakupa ujumbe wa kukuonya kuwa faili unalojaribu kulidownoad linaweza kuharibu kifaa chako, usihofu android wameweka onyo hili kwa application zote utakazojaribu kudownload nje ya playstore. Baada ya kumaliza kudownload, funga hilo faili (hapa inategemea na kivinjari chako na sehemu uliposet mafaili yote ya kupakua yahifadhiwe), litakuletea ujumbe wa kukataza kuinstall application nje ya google play, bonyeza “Go to settings” na washa au ruhusu kwa kuwasha kitufe cha “Unknown Sources”, kumbuka kuzima hii mara baada tu ya kuinstall tubemate sababu ni mwanya wa virusi kuingia katika simu yako.
Step 3: Unaweza ukatumia antivirus uliyoinstall katika simu yako kuliscan lile faili la .apk ulilodownload kabla ya kulisntall au unaweza ukaliinstall bila kuliscan kama unajiamini. Baada ya hapo utaendelea na zoezi la kuinstall Tubemate kwa kupitia hatua chache mpaka pale itakapomaliza. Baada ya kumaliza fungua application yako kwa kubonyeza icon iliyotokea katika home screen yako au katika sehemu ya applications.
Step 4: Unaweza ukaset baadhi ya settings kulingana na mahitaji yako, ila pale inapofunguka tu itakuletea orodha ya video kama ile ya youtube, unaweza ukatafuta video yoyote ile kutoka youtube hapo kwa kubonyeza eneo la kutafuta (search). Tafuta video unayotaka kuipakua, kwa juu utaona mshale wa kijani unaoelekea chini, bofya hapo na tubemate itakupa machaguo tofauti ya ubora wa video hivyo utachagua kulingana na mahitaji yako. Hapo kuna mpaka chaguo la MP3 kama utapenda kupakua audio, kisha bonyeza “Download” chini kabisa.
Step 5: Baada tu ya kubonyeza download tubmate itaanza kupakua video uliyoichagua, itakapomaliza utaiona katika notification area (uzi wa juu) na unaweza ukagusa hapo ili kuifungua na kuiangalia. Pia video itajihifadhi yenyewe kwenye gallery kwa ajili ya matumizi ya baadae, unaweza ukaituma whatsapp au kuishare facebook bila shida yoyote.
Je, una swali lolote kuhusiana na tubemate? Tafadhali uliza swali lako kupitia sehemu ya maoni ili upate kujibiwa, usisite kushare hii kwa watu unaowapenda ili wajifunze kupakua video wanazozipenda bila tabu. Riyadi Bhai ni rafiki wa wote wakati wote

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa