JINSI YA KUTUMIA FLASH DISK KAMA PASSWORD YA COMPUTER YAKO

Habari ni wakati mwingine tena leo ningependa kushare na nyie jinsi ya kutumia flash yako kama ufunguo wa kompyuta yako au password, Basi kwa kuanza basi ni vyema tukajua faida za kuwa na password katika flash drive, kuwa na password kwenye flash drive hii ina kusaidia hasa pale unapokuwa unasahau kwani tunakubaliana kuwa kuna wakati mtu unakua unasahau password tena kuzingatia kwa sasa karibia kila kitu kinatumia password kuanzia email mpaka simu yako ya mkononi hivyo basi ni rahisi sana kuwa na kumbukumbu ya mahali ilipo flash yako zaidi ya kukumbuka password ya kila kifaa unachotumia. Pia ni rahisi sana kutumia kwani hakuna haja ya kutafuta sehemu ya kuweka password bali unachokifanya ni kuchomeka flash yako tu basi hapo utakua umepata uwezo wa kutumia kompyuta yako kirahisi kabisa.

Basi tukiwa tumesha jua hayo machache moja kwa moja twende tuka jifunze namna ya kutumia flash drive kama password ya kuwasha kompyuta yako, ili uweze kufanya haya unachohitaji ni flash na internet angalau MB100 ili kuweza kupakua programu hiyo ya ku-wezesha kutumia flash kama password ya kompyuta yako.

KUMBUKA : Huna haja ya ku-format flash yako bali hakikisha flash yako ina nafasi kidogo kama MB200 hivi au zaidi

Kwa kuanza basi cha kwanza bofya link hii hapa Download kisha pakua programu ya predator na ufanye installation kwenye kompyuta yako kumbuka kompyuta yako itaendelea kuwa on endapo flash yako itakuwa imechomekwa kwenye kompyuta yako pale unapoitoa flash yako kompyuta yako huzima moja kwa moja na kuonyesha ishara ya kuwa mtumiaji hana uwezo wa kutumia kompyuta hiyo.

Basi ukisha pakua programu hiyo install kwenye kompyuta yako baada ya hapo chomeka flash yako pale programu itakapo hitaji, kisha chagua password yako na kisha bofya save. Hapo utakuwa umefanikiwa kuweka password kwenye kompyuta yako kwa kutumia flash.


Ukisha maliza vyote hivyo kama imetokea unataka ku unstall programu hii hakikisha flash inakuwa imechomekwa katika mashine yako kisha ndo uondoe programu hiyo kwenye kompyuta yako.

Kama umependa hii unaweza kushare na marafiki na kama unataka mafunzo zaidi kuhusu tech tembelea mtandao huu kila siku ili kujifunza mambo mengine mengi yanayohusu teknolojia.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa