JINSI YA KU-UPDATE TECNO C8 KWENDA KATIKA TOLEO JIPYA LA ANDROID MARSHMALLOW

T ecno C8 imekuwa simu ya pili kutoka katika kampuni ya Tecno kupokea toleo jipya la Android Marshmallow na HiOS baada ya ile Boom J8.


Tecno Camon C8, sasa rasmi imeboreshwa kwa Marshmallow ili kuweza ku-update simu yako ya Tecno Camon C8 kuna njia mbili kuu za kutumia, njia ya SD Card na njia ya flashtool. Njia inayoshauriwa na ya rahisi zaidi ni ya SD Card.
Tafadhali soma kwa makini hatua zote, kabla ya kuanza ku-update simu yako, kwani ukikosea unaweza ukaharibu simu yako (Usiwe na shaka ila kuwa makini na fuata hatua zote kama zilivyoelekezwa) . Kama itakushinda, unaweza wasiliana nasi katika sehemu ya maoni au kwa kututumia message katika ukurasa wetu wa Facebook.
NAMNA YA KU-UPGRADE TECNO CAMON C8 KWENDA MARSHMALLOW UKITUMIA NJIA YA SD CARD
1. Download Tcard_update_20160425 kutoka kwenye linki hii, hii ni kutoka katika mtandao wa tecnospot
(Unapaswa kuwa umesajiliwa ili linki hii ifanye kazi, jisajili katika sehemu ya usajili), Faili utakalo-download lina zaidi ya MB800, itakubidi uwe na internet yenye kasi na kifurushi cha kutosha.
2. Ingiza Tcard_update_20160415 kwenye SD Card yako usiingize ndani ya folder lolote, kwa maana nyingine weka katika root.
3.Fanya ‘BACKUP’ ya data zako kisha zima simu yako ya Tecno Camon C8.
4. Shikilia Batani ya kuwashia na Batani ya kuongezea sauti. Hapo nembo (logo) ya ‘startup’ ikitokea, achia Batani moja ya Kuwashia tu. Kisha utaona nembo (logo) ya android kama inavyoonekana hapo chini. Hapo Achia Batani ya kuongezea sauti.


5. Shikilia tena Batani ya Kuwashia kwa sekunde 2, kisha Bonyeza Batani ya Kuongezea sauti.
6. Tumia Batani ya Kupunguzia Sauti kwenda kutumia update kutoka kwenye SD Card kisha CHAGUA kwa kubonyeza Batani ya Kuwashia. Fanya hivyo bila kuachia batani ya kuwashia utaona uso wa simu yako yako kama inavyoonekana hapo chini.
7. Utaingia kwenye sura au uso mpya yaani ”New interface” Kama inavyoonekana hapo chini. Tumia Batani ya kupunguzia sauti kwenda kwenye Tcard_update_20160415 chagua kwa kutumia Batani ya Kuwashia
8. Hapo ‘Installation’ itaanza na ikishakamilika utaona uso ”interfcae’ ya simu yako kama inavyoonekana hapo chini. Kisha chagua Reboot system now.

9. Simu itajianzisha yaani itaji-reboot/Restart. Hapo itachukua muda hadi dakika 5 mpaka 10
10. Baada ya kukamilika kwa hatua ya simu kujianzisha yaani ”reboot process”, Fanya marekebisho ya simu yaliyokuwapo awali kutoka kiwandani yaani fanya ‘Factory Reset ili kuhakikisha hupati tatizo lolote.
Pia baada ya hatua ya reboot kukamilika unapaswa uwe na HiOS na Marshmallow 6.0 kwenye simu yako ya Tecno Camon C8.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa