MAMBO MATANO MAPYA KWENYE INSTAGRAM AMBAYO WATU WENGI HAWAYAJUI

Instagram ni moja ya mtandao wa kijamii ambao unatumiwa na watu zaidi ya billioni moja. Kwenye playstore peke yake instagram imekuwa downloaded zaidi ya mara billioni moja.

Watu wengi wanatumia instagram kila siku lakini yapo mambo mengi mapya ambayo wengi wetu bado hatuja yafahamu. Leo ntaelezea mambo matano mapya ambayo instagram wameanzisha ndani ya mwaka 2017 na baadhi ni ya mwaka 2016.

Live Stories



 Sasa kwenye Instagram utaweza kujichukua au kuji record live na watu ambao wame kufollow wakawa wanakuona live. Watu wataweza ku comment huku video yako ikiwa live. 

Saved Post

Instagram inatumbua kwamba watu wapo busy, sasa inakupa uwezo wa ku save post ambayo ungependa uje uingalie baadae. Ku save post ni kitu rahisi sana. Unacho takiwa kufanya ni kubonyeza alama ya bookmark ambayo inakuwa chini ya post. Tazama picha chini kuelewa zaidi

Instagram Strories

Stories ni kitu ambacho watu wengi sana wanasema Instagram ame copy kutoka snapchat. Stories inakusanya matukio yako yote ya siku moja na watu wanaweza wakaona vitu vyote ulivyofanya siku nzima kwa pamoja. 

Event Channels

Sasa unaweza kucheck matukio kama concert za wasanii mbalimbali kupitia instagram. Hii channel inakusanya video kali kutoka kwenye matamasha mbalimbali. Kwa sasa Event Channel inaonekana kwa watu wa marekani tu. Instagram wanajitahidi kuisambaza event channels ziweze kuonekana ulemwenguni kote. 

Account Mbili

Kujua kuhusu account tatu za instagram unaweza tembelea link chini HAPA

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa