Zifuatazo Ni Application Tano Bora za Antivirus Ambazo Zitaweza Kuilinda Simu yako Dhidi ya Uharibifu Kutokana Na Virus.
1.Avast Antivirus.
Avast Antivirus Ni Moja ya Antivirus maarufu sana na Moja ya Sababu ni Ya Umaarufu Huo kutokana na Kuwa na Version ya PC Ambayo nayo imekua Ikifanya Vizuri Katika Ulinzi wa Kumpyuta. Avast Katika Android ina watumiaji Takribani Milioni 100 ambao kati yao Millioni 4 wameweza kuipa Hadhi ya Nyota 4.5 Kutokana ya Ubora wake Mkubwa.
Avast inakuja na Features mbalimbali Kama ‘Device Scanning’(Huilinda simu yako kwa ujumla dhidi ya Virus), ‘Apps Scanning’(Huskani Ili kuondoa Apps zisizo samala), ‘Anti-Theft’(Hukusaidia Pale simu yako inapoibiwa), ‘Remote Lock Your device’(Utaweza Kuifunga simu yako Endapo Imeibiwa) na Pia ‘Data base Update'(Data base yake Hujiupdate kila mara Ili kuwa ya Kisasa Kila Mara)
Avast Antivirus inapatikana PlayStore Bofya Hapa Ili Kui’Download’ kutoka PlayStore
2. AVG Antivirus
AVG Antivirus Ni Maarufu Pia Kwa watumiaji Wengi wa Kompyuta na Pia imekua ikifanya vyema katika Suala Zima la Ulinzi wa Simu Za Android.AVG Antivirus Inakuja na Features mbalimbali kama ‘Device Scanning Scan’(Kuilinda simu yako kwa ujumla dhidi ya Virus), ‘Apps Scanning’(Huskani Ili kuondoa Apps zisizo samala), ‘Anti-Theft’(Hukusaidia Pale simu yako inapoibiwa), ‘Remote Lock Your device’(Utaweza Kuifunga simu yako Endapo Imeibiwa) na Pia ‘Data base Update'(Data base yake Hujiupdate kila mara Ili kuwa ya Kisasa Kila Mara.
Kuongezea Juu ya Hayo, AVG Antivirus Inakuja na Features nyingine kama ‘Task Killer’, (Ambayo inakuwezesha Kubajeti Maisha ya betry yako Pia KuBajeti Nafasi katika Simu yako), ‘Remote Device Data Wiping’ (Inakuwezesha kufuta Data Zako Katika Simu Pindi Unapoibiwa Simu yako).
AVG Antivirus Inapatikana PlayStore Bofya Hapa Ili Kui’Download Kutoka PlayStore.
Related Article
3. 360 Security
360 Security Ni Antivirus Bora ya Android Yenye watumiaji wengi Zaidi Kufikia Takribani ya Watumiaji Millioni 200, Huku watumiaji Millioni 15 Wakiipa Application Hii Hadhi ya Nyota 4.6.
360 Security Inakuja na Features Nyingi mbalimbali Kama Vile ‘File scan‘(Kukagua File Moja Moja kama Lina Virusi), Real Time Protection’ (Hukulinda Kila Muda Uitumiapo Simu yako), ‘App Lock’(Inakuwezesha Kufunga Apps zako kwa Password’), Smart Battery Saver’ (Hukuwezesha kutunza Chaji ya Betry yako zaidi), 360 Security Pia Inakuja na ‘Booster’ pamoja na ‘Cleaner’ ambavyo Vyote kwa Pamoja Huongeza na Kuimarisha Utendaji wa Simu yako.
360 Security Inapatikana PlayStore Buree, Bofya Hapa Kui’Download’ Kutoka PlayStore
4. Kaspersky Antivirus.
Kaspersky Antivirus, Ni moja ya Antivirus Bora za Android ambayo Ni Rahisi Kutumia na Inapatika Bure Play Store. Kaspersky Antivirus Ni Antivirus yenye Nguvu Hivyo Huhitaji Simu yenye Processor na RAM Kubwa Ili Iweze kufanya kazi katika Simu Husika.
Kaspersky Antivirus Inakuja Na features kama ‘Scanning’, ‘Anti-Phishing‘(Hukulinda dhidi ya Udokozi), ‘Cloud Protection’, ‘Ant-Theft’, Pia na Feature Nyingine Kama Kufanya Simu Kutoa Mlio wa Alarm Ili kukusaidia Kutafuta Simu yako Pale Inapoibiwa.
Kaspersky Antivirus Inapatikana PlayStore Bofya Hapa Kui’Download’ Kutoka PlayStore
5. McAfee Antivirus
McAfee Antivirus Ni moja kati ya Ant virus Zenye Majina Makubwa, Na Uzuri wa McAfee Antivirus Hakuna Tofauti Kubwa Kati Features za Kulipia Na Zile Za Bure.
Katika App Hii Unapata Features Nyingi za Bure Zinazokupa Ulinzi wa Kutosha, Japo Baada ya kulipia Utapata Features za Ziada Kama ‘Power Booster’ Ambayo Unaweza Achana nayo Sababu Free Version imetoa Ulinzi wa Kutosha. McAfee Antivirus Inapatikana PlayStore Buree Bofya Hapa Ili Kui’Download’ Kutoka PlayStore.
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa