Jinsi ya kutumia simu yako kama modem bila kuwasha WIFI

Habari ndugu msomaji wa blog hii Riyadibhai.com leo nimekuja na jambo hili dogo kwa wanaolifahamu lakini ni kubwa kwa wasio lifahamu , kutokana na kuhangaika kwa siku taku baada ya modem yangu kupata shida ndio nikapata akili hii ambayo naenda kukufahamisha na wewe ili usipate tabu kama niliyoipata mimi Tuanze.


ili uweze kutumia simu yako kama modem kwanza hakikisha unakuwa na USB WIRE kisha fuata hatua hizi

Chomeka USB WIRE kwenye computer/laptop kisha chomeka na kwenye simu yako nenda kwenye setting ya simu yako


kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa More...
 Kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Tethering & portable hotspot  
Kisha weka alama ya Tiki kwenye sehemu iliyoandikwa USB tethering kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu kisha utasubiri kwa sekunde kama tano hivi ili mashine yako ifanye mchakato wake.

mpaka hapo sasa furahia Internet yako bila kuwa na modem, niachie maoni yako hapo chini kama imekusaidia au kama haijakusaidia makala hii nikuelekeze zaidi. share makala hii kwa marafiki kadri uwezavyo

 mpaka hapo

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa