Jinsi ya kutambua processor ya simu na kuijua simu ghushi(AndroidOS)


Processor katika simu ni kifaa ambacho huchukua maelezo kutoka kwenye software na kufanya kazi za kimahesabu na kimantiki pamoja na kutoa na kuingiza vitu ili simu yako ifanye kazi kwa ufanisi. unapo peruzi internet au kuangalia video na picha basi processor inakuwezesha. tunaweza kusema ni moja kati ya vitu muhimu kwenye simu na processor ikiwa nzuri na simu itakua nzuri pia.

karibia simu zote zinatumia processor za arm ambazo zimetengenezwa huko uingereza. makampuni kama qualcom, samsung na apple hutumia chip za arm na kudesign wanavyotaka wao na leo hii unakuta soc kama exynos, tegra na snapdragon.

aina za processor
hawa arm wana series yao ya processor inayoitwa A series ambayo ndio sana inatumika kwenye simu na inajumuisha processor hizi.
-cortex A5
-cortex A6
-cortex A7
-cortex A8
-cortex A9
-cortex A12
-cortex A15

processor hizi ndio kama unavyosema intel i3, i5 au i7. kama nilivyozipanga hapo juu cortex A5 ndio ndogo na cortex A15 ni kubwa. hivyo unapochagua proccessor za simu usiangalie clock speed kwanza mpaka uangalie aina ya processor. mfano processor ya 1.2ghz quadcore cortex A7 imepitwa nguvu na 1ghz dualcore cortexA15.

jinsi ya kutambua simu yako inatumia processor ipi
kuna njia mbili hapa za kujua.
1. kuangalia specs online. hapa unaweza kwenda website kama gsmarena halafu ukachagua simu yako na kuangalia specification
2. kwa kuinstall app halafu kujua specs za simu kutumia hio app mfano cpu-z

jinsi ya kutambua simu fake
combination ya njia zote mbili hapo juu itakufanya ujue simu zote fake na original. 

mfano hapa nita assume mtu ameniletea samsung galaxy s3 ili niitambue kama ni fake au original. kwanza nitaenda gsmarena na kuangalia specs zake,

 hapo utaona s3 ina chip inaitwa exynos na processor yake ni cortex A9 quadcore 1.4ghz

halafu nitainstall cpu-z kwenye hio simu na kukagua specs zake.
 hivyo hapo juu utaona kuwa specs za gsmarena na cpu-z zimefanana na kuonesha simu ni original. zingekua tofauti hapo unajua simu sio umepigwa changa la macho. nafkiri hii itasaidia wale wote wanaotaka kujua simu fake na original

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa