[soma Njia za kupata pesa kupitia adsense kwenye blog/website yako]
Jambo la msingi ambalo tunapaswa kufahamu ni kuwa Google Adsense ni programu ya kibiashara zaidi kwa maana google wanaangalia zaidi maslahi yao kutoka kwa makampuni na wafanyabiashara wanaohitaji matangazo yao yaonekane mtandaoni.
Je umewahi kujua kwamba nyuma ya Google Adsense kuna programu inayohusu wamiliki wa matangazo iitwayo Google Adwords.Programu hii inawapa wamiliki wa matangazo uwanja wa kuchagua aina ya website au blog ambazo wangependa matangazo yao yaonekane.
Miongoni mwa vigezo ambavyo wamiliki wa matangazo huangalia katika kuomba kutangaziwa bidhaa au huduma zao kupitia google ni:
- Maneno ya msingi (Targeted Keywords)
- Eneo au Nchi (Geographical Location)
- Lugha itumiwayo katika Website (Language)
HIVI NDIVYO VIKWAZO VYA LUGHA YA KISWAHILI
1.wamiliki wa matangazo
Ikiwa umefanya uchunguzi wa kina katika matangazo ya Adsense yanayomilikiwa na makampuni ya tanzania,ASILIMIA 90utagundua kuwa ni wamIliki wa mitandao ya simu….FANYA UCHUNGUZI.Hii ni kutokana na makampuni haya huchagua eneo au nchi ambazo wanataka matangazo yao yaonekane “geographical location” na sio “targeted keywords”
Ukiwa kama blogger mwenzangu nikupe siri ya kuwa wanaokiangusha kiswahili katika programu ya adsense ni wamiliki wa matangazo.Hii ni kutokana na Programu ya Google Adwords inawapasa wamiliki wa matangazo kuchagua maneno ya msingi “keywords” ambayo matangazo yao yataonekana katika blog zilizobeba hizo “keywords”
2.“Target keyword”
Katika programu ya google Adsense tunapoongelea “Keyword” tunamaanisha yale maneno ya msingi yanayopatikana katika utafutaji ndani yagoogle.com.Ukilinganisha takwimu za utafutaji wa “keywords” ndani ya google.com utaona utofauti mkubwa wa lugha ya kiswahili na lugha nyingine.
Mfano mtu anayeandika kwa lugha ya kiingereza kupitia google “how to get diabetes treatment” hapa utaona “keywords” ni “diabetes” na “treatment” ambapo kwa lugha ya kiswahili mtu anayetafuta jambo lile lile angeandika “namna ya kupata matibabu ya ugonjwa wa kisukari” hivyo hivyo pia utaona “keywords” hapa ni neno “matibabu” na “ugonjwa wa kisukari“.
Kwa mfano mdogo hapo juu utaona ya kuwa hakuna kampuni nchini Tanzania au hata duniani itakayo iomba google iweke matangazo yake katika blog zinazozungumzia “ugonjwa wa kisukari” ukilinganisha na “keyword” kama “diabetes” ambayo ina maana sawa na ugonjwa wa kisukari.
Makampuni mengi makubwa yanatarajia wanapoweka matangazo yao katika “targeted keywords” ni rahisi kumshawishi mtumiaji ku bofya “click” tangazo lao kwa maana hiyo ujumbe wao utakuwa umemfikia mlengwa.
Kulingana na hili pia jaribu kufanya uchunguzi katika blog au website nyingi za kiswahili,wengi wao wanazungumzia habari ,matukio,udaku na michezon tu.Hivi ni kweli kuna kampuni gani ya nje itakayokubali kuweka tangazo lao katika blog yenye habari tu.Hii ni kutokana na kuwa hakuna kampuni inayouza bidhaa zinazohusiana na habari.
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa