Whatsapp kuja na feature ya kutumia akaunti zaidi ya moja kwenye simu moja

 Whatsapp sasa wanataka kuleta feature ya kuweza kutumia akaunti ya Whatsapp zaidi ya moja kwenye simu Yako bila kutumia simu nyingine au kuigiwa Whatsapp mara mbili.


Watumiaji wa Whatsapp business na Whatsapp messenger ambao wamejiunga na beta muda sio mrefu watakua na uwezo wa kuchagua akaunti zaidi ya moja kwenye Whatsapp bila kubadilisha simu nyingine.

Au kutumia simu nyingine ambapo utakua na uwezo wa kuunganisha akaunti zaidi ya moja bila shida yoyote. 


Kwaiyo watumiaji wa Whatsapp beta watakua na uwezo wa kutumia akaunti zaidi ya moja kwenye Whatsapp moja kama ilivyo  Insta, Facebook, Twitter, TikTok nk.

Ile tabia ya kuifanya Whatsapp kuwa dual app au kutumia simu nyingine kuunganisha Whatsapp zaidi ya moja itakua mwisho.


Kwani  ndani ya simu Yako  utakua na uwezo wa kuunganisha akaunti za Whatsapp zaidi ya moja.


0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa