Dunia ilionekana kuwa tulivu bila wewe.
Ni mwaka wa 12 sasa umepita tangu uondoke kwenye ulimwengu huu bado ninakuombea kila siku. Inazidi kuwa ngumu kwangu hii dunia kukaa katika hali njema.
Usiku na mchana wangu umejawa na mawazo ambayo hayawezi kuzuilika, yananichosha na ninatamani ungekuwa hapa basi labda kila kitu kingekuwa sawa kwa sababu nimechoka sana kuwa hapa, ulimwengu huu haufanani na kitu chochote cha kupendeza bila wewe.
Ulikuwa mwanadamu mkarimu zaidi, ulimwengu huu haukuwahi kustahili mtu wa thamani kama wewe kwangu.
Naomba tukutane tena Jannah na kamwe tusipate maumivu ya kupotezana tena.
ni mimi Ibrahim Riyad
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa