Simu hizo zilizoondolewa sokoni, na ambazo pia zimefutwa rasmi katika tovuti ya Apple ni pamoja na iPhone 6S na iPhone SE, hiyo ikimaanisha kuwa sasa huwezi tena kununua iPhone yenye sehemu ya kuchomeka spika za masikioni ukubwa wa milimita 3.5.
![]() |
Mojawapo ya iPhone ambazo Apple wametangaza kuachana nazo na hatua hyo ni kwamba unaweza kununua hizo simu katika maduka mengine na si katika tovuti rasmi ya Apple. |
Na pia kama ulikuwa unasubiri kuchaji simu yako mpya ya iPhone katika AirPower mat, utapaswa kusubiri hadi Septemba 21 mwaka huu wakati Chaji Qi isiyotumia waya itakapotolewa rasmi kwingineko duniani baada ya kuzinduliwa Septemba 14.
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa