As salaam Aleikum ndugu mtenbeleaji wa blog yetu hii miezi kadhaa nyuma tuliandika makala kwaajili yako kuhusu Seebait jambo ambalo limewasaidia watu wengi sana kujua ni namna gani au Jinsi ya kujiunga na seebait, lakini kutokana na makala yetu hiyo watu walikuwa na maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu seebait ivo tukaandaa makala nyingine ambayo tulielezea mambo usiyoyajua kuhusu seebait lakini kiu ya wapenzi wasomaji wetu wa blog hii na wanaopenda kujua zaidi kuhusu seebait

Basi leo tupo hapa kumaliza kiu ya kila mmoja wenu ambae anapata ukakasi kuhusu seebait tutajaribu kuelezea kwa undani zaidi kuhusu seebait kwa masaada wa seebait wenyewe.

1. ni kipi kiwango cha chini cha malipo?Kiwango cha chini ambacho seebait wanawalipa mawakala wao ni USD 50 (pesa zote kwenye mtandao wa seebait zipo kwa pesa/sarafu za dola ya Marekani).

2. ni njia ipi ya kuweza kupokea malipo?Kwa kawaida huwa malipo yanafanyika kwa njia ya bank transfers maana pesa zote wanazolipwa huwa zinapelekwa benki na hivyo zoezi la malipo inakuwa rahisi kulipa kupitia benki. Ila kama mtu hana account ya bank anaweza kulipwa kupitia mitandao ya simu, cha muhimu ni awe ameweka hayo maelezo kwenye account yake ya seebait sehemu ya Bank Account Details kwenye page hii https://seebait.com/publisher/profile (baada ya kuingia kama blogger/publisher).
   
3. malipo kiasi gani kwa user wangapi?Kiasi wanacholipa na idadi ya watu wanalipa kinategemea na mambo megi ikiwemo kiasi wanalicholipwa, watu wangapi waliolipa na kiasi gani kinadaiwa. Ila kwa ukawaida huwa wanapitia maombi yote ya pesa na kutoa waliojirudia zaidi ya mara moja au kuchagua kiasi cha juu kilichoombwa kwa watu waliojirudia kisha tunalipa ikitokea pesa zimeisha kabla hawatujalipa watu wote walioomba basi wanapolipwa tena hao ndio wanapewa kipaumbele, cha kuzingatia ni watu wajue kuwa seebait huwa hailipwi kabla kazi haijaanza maana kuna vitu inatakiwa wakamilishe ili mteja alipe mfano wafikie watu kiasi fulani, au matangazo yaonekane mara fulani au ya klikiwe mara fulani, na hapo tu wanapofikisha ndio wanaenda kwa mteja na kuanza hatua za kupokea malipo ambazo mara nyingine huchukua mpaka miezi 2, hivyo basi wadau wanapoona pesa zimechelewa ni kuwa seebait wenyewe huwa wanasubiria walipwe ili waweze kukamilisha malipo.

4. Je wanalipa kwa click au views? Seebait huwa wanalipa kwa views, pointi muhimu ni kuwa watembeleaji wako ndio mtaji wako.

5. je wanachukua muda can kuapprove blog? kwa kawaida inachukuwa masaa 8 mpaka siku 7 kutokana na idadi ya blog zinazoingia na pia watu wanaofanya approval pia wanatakiwa kuangalia ubora wa blog na kutoa mapendekezo yoyote kamayapo kisha ndo wana ruhusu ipokee matangazo

6. Je huwa wanazikubalia blog zilikuwa na muda hewani gani? Seebait huwa wanakubali blog hata kama imeanzisha siku hiyo hiyo, cha muhimu ni ubora wake na maudhui ya blog husika, ndio maana kuna kipindi cha fall back(Fallback Period) ni kipindi kimewekwa maalum kwa ajili ya kuangalia blog inafanya vipi na inaongezea vipi mzigo kwenye miundo mbinu ya seebait kabla haijaanza kupokea matangazo ya makampuni ambayo yanalipiwa.


Neno kutoka kwa seebait.com
Ningependa pia kutumia nafasi hii kukumbushia kuwa tunaomba watu wanapofanya maombi ya pesa wasubirie mpaka yafanyiwe kazi ndio waombe tena maana kuomba mara nyingi nyingi muda mwingine ndio hupelekea mchakato mzima wa kulipa ukachukua muda mrefu maana unakuta maombi zaidi ya robo ni ya kukatalia na pia kwasababu tunafanya kazi na pesa watu waliofanyia kazi inabidi umakini uwe wa hali ya juu kuepuka mtu kupunjwa pesa zake.

Asante sana.

Bila shaka umepata machache kati ya mengi kuhusu seebait kama bado kuna mengine unatamani kuyajua au yanakusumbua kuhusu seebait basi sisi tupo kwaajili yako dondosha coment yako katika maoni hapo nasi tutakujibu kwa uhakika zaidi na kwaharaka, sambaza upendo kwa kushare makala hii kwa marafiki.
Axact

Ibrahim Riyad Houmud

As Salaam Aleikum, I'm Ibrahim Riyadi Houmud, Founder and CEO of RiyadiBhai blog from Mororgoro, Tanzania. I started this blog as a Passion and it now empowering thousands of readers around the globe.Here I usually share news, Adsense tips, wordpress, gadget, widget, Themes, windows, etc.

Post A Comment:

0 comments:

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa