Instagram Yaongeza Kipengele cha Shopping Kwenye Stories

Wakati mtandao wa Instagram ukiwa kwenye hatua za awali za kuja na programu maalum ya kununua bidhaa kwa kupitia akaunti za Instagram, Kampuni ya Facebook kupitia mtandao wa huo wa Instagram hivi juzi imetangaza kuja na njia mpya ya kuweza kurahisha watu kununua bidhaa moja kwa moja kupitia kwenye app ya Instagram.

Kupitia sehemu ya Stories, Instagram inategemea kuleta sehemu mpya ya Shopping ambayo itakuwa kwenye sehemu ya Explore iliyotambulishwa hivi karibuni ambapo Kupitia sehemu hiyo ya Stories utaweza kuona bidhaa mbalimbali zikiwa zimewekewa stika ambazo utakapo bofya hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye tovuti yenye bidhaa uliyo iona kupitia sehemu hiyo ya Stories.
Kama unavyoweza kuona sehemu hiyo kwenye picha hapo juu, pale utakapo bofya sehemu ya Shopping Explore utaweza kuona bidhaa nyingi kutoka kwenye akaunti mbalimbali ndani ya mtandao wa Instagram. Mbali ya hayo pia watumiaji wa mtandao huo watapewa uwezo wa kuuza bidhaa mbalimbali kwa urahisi kwa kuweka stika ya Shopping ambayo itapatikana kwenye sehemu ya Stika kwenye sehemu ya Stories.

Sehemu hii inatarajiwa kuwafikia watumiaji mbalimbali kuanzia siku ya leo hivyo hakikisha unasasisha (update) toleo jipya la App ya Instagram kupitia masoko ya Play Store na App Store.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa