Seebait.com,
moja ya makampuni yanayoongoza katika matangazo ya mtandaoni,
imechaguliwa kuwania nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika tuzo
zijulikanazo kama Southern Africa Startup Awards.
Taarifa
iliyotolewa na msemaji wa Seebait Jijini Dar es Salaam, ilisema kuwa
Seebait imechaguliwa kati ya washindani wengine 3200.
Alisema
walichaguliwa na majaji na wataalamu kuwa miongoni mwa makampuni
mengine ili wapate nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika kipengele
kimoja kati ya 14 katika Tuzo hizo zitakazofanyika Novemba 21 na 22
mwaka huu huko Johannesburg, Afrika Kusini.
Alitoa
rai kwa watanzania wawapigie kura kwa wingi ili Seebait ipate nafasi
hiyo muhimu katika Tuzo hizo za kwanza kuandaliwa na Southern African
Start Up Awards.
Kwa watakaotaka kupiga kura, wanatakiwa kwa mujibu wa msemaji kutembelea
Related Article
Alisema
upigaji kura umeanza rasmi na zoezi hilo litakamilika siku ya Ijumaa
Septemba 4 na kuwa matokeo yatatangazwa na jopo la majaji waliochaguliwa
kila nchi ili kupata washindani wa kila kipengele ambao watawakilisha
nchi zao katika ngazi za kanda na pengine katika hatua ya dunia.
Kwa
mujibu wa Southern African Start Up Awards, kutakuwa na kipengele cha
Shirika ambalo ni Chaguo la watu (People’s Choice Category).
“Matokeo yatatangazwa na wabia wa Southern Africa Start Up Awards mara baada ya upigaji kura kukamilika,” alisema.
Seebait
ilianzishwa mwaka 2015 kama kiunganishi kati ya watoa matangazo na
wenye majukwaa mbalimbali kama tovuti na blogs ili kuhakikisha
watangazaji wanapata jukwaa kubwa zaidi la kutangaza bidhaa au huduma
zao na wenye majukwaa haya wanapata wasaa mzuri wa kuandaa maudhui bora
kwa watembeleaji wao, pia wakitangaza bidhaa na huduma mbali mbali
kupitia majukwaa yao na kupata stahiki zao vikamilifu.
seebait.com inashikilia nafasi ya kwanza kwa Tanzania kwenye chati za Global start up ranking,
Tembelea www.seebait.com kujua mengi.
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa