JINSI YA KURUDISHA KAZI ILIYOPOTEA KATIKA MS OFFICE

As salaam aleikum mpendwa msomaji wangu, Kuna siku nilikuwa naandika makala moja nzuri na ndefu kwa ajili ya kuipublish kwenye swahilitech, nikiwa kama page ya tano ghafla umeme ukakatika na nisijue nini cha kufanya sababu kazi yenyewe nilikuwa sijaisave (hifadhi) bado.
Nadhani hata wewe ulishawahi kukutwa na aina hii ya fedheha na ukashindwa kujua nini cha kufanya. Ondoa shaka leo nitakuelekeza jinsi ya kurudisha kazi yako uliyoifunga kwa bahati mbaya au kwa sababu ya kukatika kwa umeme katika Microsoft Word, Microsoft Publisher, Microsoft Excell pamoja na Microsoft Power Point. [soma : Activate microsoft office free download ]

Njia hii inafanya kazi vizuri zaidi kwa vifurushi (packages) za Microsoft Office 2010,2013  na 2016 kwa sababu kazi unayoichapa huwa inahifadhiwa kwenye draft bila ya wewe kujua. Unaweza ukaset muda wa kazi kuwa saved automatically katika Tab ya save, ila kwa kawaida huwa inakuwa ni dakika 10.
[soma : microsoft office professional plus 2016 product keys, serial keys 2017 ]
Njia za kufuata ili kurudisha kazi yako uliyoifunga kwa bahati mbaya katika moja ya bidhaa za Ms Office

  1. Fungua Microsoft Office uliyokuwa ukitumia kama ni Word, Excel, Publisher au Power point
  2. Bonyeza File Tab, upande wa kushoto juu kabisa, kisha bonyeza Recent
  3. Bonyeza Recover Unsaved Document kama upo kwenye Ms Word, na Recover Unsaved Workbook kama upo kwenye Excel na Recover Unsaved Presentation kama upo kwenye power point.
  4. Kazi yako iliyohifadhiwa kwenye draft itaonekana na utaifungua ili kuendelea kuiedit (kuifanyia kazi)
  5. Baada ya kuifungua sasa kumbuka kuisave ili kupunguza uwezekano wa kuipoteza tena pale umeme unapokatika.
Nadhani sasa utakuwa umefahamu jinsi ya kurudisha kazi yako iliyopotea kwa bahati mbaya, na kama ulikuwa unaandika makala au unachapa kazi ndefu nadhani una kila sababu yakufurahia.

sambaza upendo kwa kushare makala hii kwa washkaji ili nao wasihuzunike na hadha za kupoteza kazi zao

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa