UC BROWSER YAREJEA TENA PLAY STORE BAADA YA KUREKEBISHWA MAKOSA

Hatimaye wapenzi wa kivinjari cha UC Browser sasa wanaweza kuendelea kufurahia kivinjari hicho mara baada ya kurudishwa kwenye soko la Play Store.
Kivinjari hicho kilitolewa na Google kutoka kwenye soko la Play Store siku chache zilizopita, huku kikiwa kinashutumia kwa makosa mbalimbali ikiwa pamoja na ile ya kuwa kivinjari hicho hutuma data za watumiaji wake bila ruhusa kwenda nchini china pamoja na kuvunja sheria za soko la Play Store
Aidha pamoja na hayo wahusika wa kivinjari hicho kutoka kampuni ya UC Union, wiki hii walitangaza kuwa sababu za kuondolewa kwa kivinjari hicho ni kutokana na aina fulani za mpangilio (settings) zilizokuwa ndani ya programu hiyo zilikua haziendani na vigezo na masharti ya google kupitia soko lake la Play Store.
Hata hivyo kampuni hiyo ilikanusha kuhusu tuhuma za kivinjari hicho kutuma data za watumiaji wake nchini china huku msemaji wa kampuni hiyo akiwataka watumiaji wake kuendelea kufurahia matumizi ya kivinjari hicho ambacho sasa kimerejea kwenye soko la Play Store.

Kivinjari cha UC Browser sio maarufu sana kwa watumiaji wengi wa Android kutokana na simu hizo kuja na kivinjari cha Google Chrome mara baada ya kununua simu hizo, lakini hata hivyo kivinjari hicho kimejizolea umaarufu mkubwa kwa nchini india pamoja na china.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa