Uwezo na Sifa za Huawei Honor 6C Pro
Kioo: 5.2-inch S-IPS, 720 x 1280 pixels (282 ppi)
Prosesa: Octa-core Mediatek MT6750 CPU na RAM 3GB
Mfumo endeshi: Android 7.0 (Nougat), EMUI 5.1
Uhifadhi: Ujazo wa ndani (Storage) 32GB , pia unaweza kuweka memori hadi 256GB
Kamera: Kamera ya nyuma (Rear) 13MP na Kamera ya mbele (Selfie) 8MP
4G LTE Data
Fingerprint Scanner
Betri: 3000 mAh Li-ion Battery
Muundo na skrini
Huawei Honor 6C Pro ina umbo la chuma. Upana wake ni milimita 7.65, ina uzito wa gramu 145 na muundo wa simu kwa ujumla ni mzuri.
Huawei Honor 6C Pro inakuja na skrini ya 5.2-inch S-IPS yenye resolution ya pixels 1,280 x 720. Ingawa hii haikupi uwezo wa kupiga picha kali zaidi, bado unaweza kufurahia-kupiga picha zinazopendeza.
Related Article
Kamera na UhifadhiKatika idara ya kamera, simu ya Huawei Pro 6C ina 13MP kwenye kamera ya nyuma na 8MP kwenye kamera ya mbele. Unapata sifa/uwezo mwingine kama vile autofocus, LED flash, HDR na uzuri wa uso ili kuongeza ubora wa shots unazochukua. Kwa shooter hii ya 8MP, mashabiki wa selfie watavutiwa zaidi.
Uwezo wa ndani wa kuhifadhi ni GB 32. Ikiwa haitoshi, Huawei Honor 6C Pro inakupa uwezo wa kuweka memori kadi hadi ya 128 GB.
Utendaji na OS
Kwa prosesa ya MediaTek MT6750, Huawei Honor 6C Pro haipaswi kufanya vibaya sana kwa bei yake, kiutendaji zaidi. CPU inafanya kazi yake kwa kiwango cha kasi ya 1.5 GHz. RAM ya uwezo wa 3GB imewekwa kuongeza ufanisi wa simu. Mfumo wa uendeshaji unaotumika kwenye simu hii ni Android 7.0 Nougat.
Sifa nyingine na Uwezo
Betri ya ujazo wa 3,000 mAh inafanya simu hii iwe na uwezo wa kukaa masaa mengi. Simu hii yenye laini mbili inakupa uunganishaji wa LTE kupitia njia zake zote mbili za SIM. Vipengele vya uunganishaji wa wireless vinapatikana kwenye Huawei Honor 6C Pro ikiwa ni pamoja na Wi-Fi yenye kasi na Wi-Fi Direct na hotspot, na Bluetooth 4.2.
Huawei Honor 6C Pro inauwezo wa USB On-The-Go (OTG). Pia ina scanner ya vidole kwa nyuma kwajili ya kuongeza usalama.
Bei na Upatikanaji
Huawei Honor 6C Pro bado haipatikani Tanzania, Kenya, na Uganda. Kwa sasa hatuna data juu ya bei na upatikanaji wake Tanzania, Kenya, na Uganda. Itakapoanza kupatikana, bei ya Huawei Honor 6C Pro nchini Tanzania inatarajiwa kuwa kati ya Tsh 470000 na Tsh 700000 kulingana na eneo lako.
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa