JINSI YA KUCONVERT FACEBOOK AKAUNTI KUWA KURASA YA KIBIASHARA

As salaam aleikum ndugu wasomaji wa blog hii leo tena katika kuendelea kupeana mawili matatu katika mambo tunayoyafahamu ili kuendelea kuongeza ufahamu wa bongo zetu leo tuzungumzie Jinsi ya kubadilisha facebook akaunti na kuwa page/kurasa

kuna mambo machache ya kujua kabla ya kufanya zoezi hili 

  1. Unaweza kubadilisha wasifu wako kwa mara moja pekee
  2. utakapobadilisha akaunti yako kuwa kurasa haitafutika ila utakuwa na akaunti yako na ukurasa wako wa facebook
  3. jina la akaunti yako ndio litakuwa jina la ukurasa
  4. facebook watakusaidia kifaa cha kuhamisha habari kutoka katika wasifu wako binafsi kwenda katika ukurasa baada ya siku 14
  5. unaweza ukachagua marafiki zako wa akaunti binafsi kuwa wamelike ukurasa wako lakini machapisho kutoka katika wasifu wako binafsi yatabakia katika wasifu.
  6. utasimamia ukurasa wako kutoka katika wasifu wako binafsi
Baada tu yakumalizika zoezi la kubadilisha wasifu wako kuwa ukurasa, wale marafiki zako wote watakuwa wame like ukurasa wako huo, ivo kama unamarafiki 1000 au zaidi basi page yako itakuwa na like 1000 au zaidi.

kama unahitaji kufanya zoezi hilo la kubadilisha wasifu binafsi kuwa page basi ni rahisi kama kutembelea blog ya Riyadibhai.blogspot.com na kunufaika zaidi bonyeza hapa https://www.facebook.com/pages/create.php?migrate fuata maelekezo utakutana na ukurasa wenye muonekano huu chini pichani
utabonyeza hapo Get Started kisha fuata maelezo mpaka mwisho lakini ukikwama usisite kuniachia maoni yako hapo chini ili nijue jinsi ya kuweza kukusaidia karibuni sana Riyadibhai.blogspot.com

2 Comments

  1. Mimi Niko na page lakini marafiki hawakuhama yaani nilianza moja kabisa FB kawaida Nina marafiki 5000 tu ila page ni followers 500 tu nataka kujua nahamisha vipi hawa marafiki waje kwenye page?

    ReplyDelete

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa