CHINA YAZUIA MTANDAO WA WHATSAPP

Watumiaji wake wamekumbwa na tatizo katika utumizi wa mtandao huo kwa zaidi ya wiki moja huku huduma ikikosekana.
Huduma ya mtandao ya WhatsApp imefungwa nchini China serikali inaimarisha usalama kabla ya kufanyika kwa mkutano wa chama cha Kikomyunisti mwezi ujao.
Watumiaji wa mtandao huu wa kijamii wamekumbwa na tatizo katika utumiajii wa mtandao huo kwa zaidi ya wiki moja huku huduma ikikosekana.
WhatsApp imezimwa na ilikuwa inaweza kupatikana kupitia mtandao wa kibinafsi wa VPN ambao unasimamia mitandao ya China pekee.
WhatsApp ni huduma ya facebook ya pekee inayoruhusiwa kurusha huduma zake nchini China. Facebook ndio huduma kubwa ya mtandao huku programu ya picha ya Instagram ikiwa pia haipatikani.
Huduma ya WhatsApp ilianza kutopatikana mtandaoni zaidi ya wiki moja iliopita. Vipimo vya huduma zake siku ya Jumanne vilionyesha kuwa watumizi wa China hawakuweza kutuma video ama hata picha kwa watu wengine nje ya China.
Uharibifu huo unafuatia masharti ya simu za Video na picha mnamo mwezi Julai, ambayo baadaye yaliondolewa.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa