Je Unaifahamu Browser maalumu kwaajili ya waislamu!? hii hapa


Katika kukaribia kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani kama wewe ni mmoja wa Waumini wa Dini ya Kiislamu basi ni muhimu kusoma makala hii.


Sasa kama ulikuwa hujui, kuna aina mpya ya browser ambayo imetengenezwa maalum kwa waumini wa dini ya kiislamu. Browser hiyo au kivinjari hicho kinakupa uwezo wewe muslamu kufanya mambo mbalimbali ambayo pengine ulikuwa huwezi kufanya kwenye browser ya kawaida.



Browser hiyo inakuja na sehemu maalum za kuonyesha muda wa kuswali, pia utaweza kupata taarifa mbalimbali za habari za dini ya kiislamu, pamoja na kujifunza maneno mbalimbali kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha Quran.



Mbali na hayo yote browser hiyo inayoitwa itakupa uwezo wa kuwa salama mtandao kwa kuzuia kutenda dhambi hasa kipindi hichi cha mwezi mtukufu kwa kutembelea tovuti ambazo hazi ruhusiwi kwa mujibu wa sheria za dini ya Kiislamu.


Endapo mtu atafungua tovuti yenye mambo ambayo yanakatazwa, kivinjari hicho kitakupa ujumbe kwamba kutembelea tovuti hiyo ni kinyume na sheria za dini ya Kiislamu.


Mbali na hayo Browser inakuja na sehemu ya kuchat ambayo inawawezesha waislamu wote kwa pamoja kuchat kwa pamoja kupitia kivinjari hicho. Uzuri wa sehemu hii ni kuwa inaweza kuku unganisha na waislamu waliopo karibu na wewe, takribani kilomita 1 toka ulipo.



Kivinjari hichi ni kuzuri sana kwa waislamu wote na inakupa muonekano mzuri na bora kama ilivyo Google Chrome, kama wewe ni baba au mama mwenye mtoto ni vyema kutumia kivinjari hichi kwani kitasaidia mtoto kukuwa kwa kufuata maadili ya dini ya Kiislamu. Kama unataka kudownload app hii inapatikana kwenye mifumo yote ya Android, iOS, macOS pamoja na Windows.



chanzo : Tanzania Tech

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa