As salaam aleikum ndugu msomaji wa blog yetu leo tudurusu kidogo katika Upande wa kijitafutia kipato kupitia blog zetu, wengi wameshahangaika sana kuhusu adsense lakini wametoka patupu Jambo ambalo limewafanya kukata tamaa kuhusu kupata pesa kupitia site zao, Mtafutaji mwenzako nipo hapa sasa nakwambia simama tuanze safari yetu ya kujitafutia mkate wa siku kupitia tovuti zetu, Hapa chini nimekuwekea orodha ya site kumi kwaajili yako

1.Media.net
Huu ni mtandao safi kwako wewe ndugu yangu mtandao huu unamilikiwa na Mtandao wa Yahoo matangazo yake ni kama ya adsense tu, Pia wanalipa kuanzia dola 100, 

Kama ulikuwa unahangaika kutafuta tovuti kama ya google adsense basi hii ndio tovuti sahihikabisa kwako, hakuna scammy ads katika tovuti hii pia unaweza kuunda tangazo linaloendana na blog yako jambo ambalo litakufanya uweze kukuza kipato chako, Hii ni moja ya tovuti kubwa ambayo inamatangazo mengi na inalipa vizuri kama adsense tu, Je unasubiri nini Kujiunga Tembelea www.Media.net

2. Infolinks.Com
Tovuti hii inaitwa Infolinks hii ni maarufusana kwa mfumo wake wa matangazo kwa njia ya maandishi Infolink huwa wanalinganisha chapisholako na tangazo lao Jambo ambalo litakusaidia wewe kupata mapato zaidi hawa jamaa wanalipa kwa click hii inamaanisha click zaidi basi ni pesa zaidi, Infolinks inamatangazo ya kutosha kwaajili yako, pia wanakulipa kupitia Paypal, Bank, Check n.k

Njia bora ya kuweza kukuza mapato yako kupitia Infolinks ni kutokuweka matangazo mengi katika kurasa moja ni vema ukaweka matangazo 6 mpaka 8 hii ndio njia nzuri ila kama utaweka mengi zaidi ya hayo niliyokuambia wenda matangazo yasionekane, Pia jishughulishe zaidi katika uandishi wa makala nzuri za kuvutia watembeleaji kwenye blog yako maana hao ndio pesa yako, sio eti kwasababu nimekwambia unaweza pata pesa ndo unawaza pesa ukasahu kuwa kazi yako ni kuwaandikia watu wako makala zenye mvuto utafeli kupata hiyo pesa na kupelekea kukimbiwa na watumiaji wa blog yako.


andika makala nzuri kisha ongeza na code za infolinks hapo utaona utamu wa makala yako hiyo ya kuvutia.

  • Infolinks ni bure na ni rahisi kabisa kwaajili ya blog yako
  • infolinks haichukui nafasi katika blog yako matangazo yake ni rahisi mno
  • hakuna ujanja ujanja ni asilimia mia kupata haki yako
Infolimks ni bora kuwa mbadala wa google adsense kwasababu hata muonekano wa matangazo yake unategemea na keyword za blog yako kama adsense ivo ni rahisi kupata mapato zaidi sababu matangazo yatakayoonekana yatawavutia watembeleaji wako, Wanalipa kuanzia dola 50, Kujiunga tembelea www.Infolinks.com


3. Chitika.com
Tovuti hii inaitwa Chitika kitu ambacho ni kikubwa ni kuwa chitika inafanan na adsense kwa asilimia kubwa sana chitika pia ina CPC Chitika inaonyesha matangazo yake kulingana na blog yako maudhui pamoja na muonekano wa blog yako.

Malipo ya nafanyika kwa njia tofauti tofauti kwa paypal ni kuanzia dola 10, lakini kwa njia ya cheki ni dola 50, pia wana affiliate program ambayo itakusaidia wewe kuongeza mapato yako kwa kila memba atakayejiunga na chitika kupitia wewe.

Chitika ni program imara yenye mawakala zaidi ya 300,000 ambao wanatumia huduma hiyo mablogger wengi wanaitumia hiyo ivo hata wewe inawezakukusaidia kupata kipato kizuri kama utafanya juhudi Kujiunga tembelea www.Chitika.com


4. Bidvertiser.com
Tovuti hii inaitwa Bidvertiser ni rahisi pia tovuti hii haina masharti kama mitandao mingine hata ukiandika kindengereko katika makala zako wao wanakukubalia tu, kiwango chao cha chini cha kukulipa ni dola 10 tu, Kujiunga tembelea www.Bidvertiser.com

5. Adsterra.com
Tovuti hii inaitwa Adsterra hii pia wanalipa vizuri pia hawachagui lugha kiwango chao cha chini cha kukulipa ni dola 100, Kujiunga tembelea ww.Adsterra.com


6. Ad-maven.com

Tovuti hii Inaitwa Admaven ni sehemu sahihi kwako kwaajili ya kjiingizia kipato mfumo wa matangazo yake ni popup and popunder bila shaka ushawahi kusikia mfumo wa popup and popunder advertising, Naam unaweza kupata pesa kwa kuwa wakala/Publisher wao, Pindi tu utakapo jisajili kama  wakala/Publisher utaona kampeni zote katika dashibodi ya akaunti yako pia utaweza kumeneji ripoti zako zote katika akaunti yako Wanamatangazo mengi na mazuri kwaajili ya blog yako.

Jinsi ya Kujiunga na Ad Maven na kuanza kupata pesa kupitia blog yako.
  • kwanza kabisa hakikisha unafungua akaunti ya ad maven kupitia link hii
  • baada ya kujisajili weka kiungo/Url ya blog yako
  • Utafahamishwa aina mbalimbali ya malipo ambapo wewe utachagua moja
  • sasa watakupatia HTML code ambazo utapachika katika tovuti yako na utaanza kupata pesa, Hakikisha popup au popunder zinafanya kazi baada ya kupachika code kutoka Ad maven, Mpaka hapo utakuwa umeshakamilisha.


7. Viglinks.com
Tovuti hii inaitwa Viglinks mfumo wake wa ni text ads yaani matangazo yake yanatokea kwa mfumo wa maandishi hawa jamaa hawana kiwango cha chini hata dola moja wanakupa unafanya yako, Kujiunga tembelea www.Viglinks.com8. Revenuehits.com
Tovuti Inaitwa Revenue Hits hii pia mfumo wake wa matangazoni wa kawaida tupia hawachagui lugha, kiwango chao cha chini ni dola 20, kujiunga Tembelea www.Revenuehits.com

9. Clicksor.com
Tovuti inaitwa Clicksor pia mfumo wake wa matangazo upo katika maandishi ila pia wa Pop up, Banner na hata Interstitial Ads kiwango chao cha chini cha kukulipa ni dola 50, Kujiunga tembelea www.clicksor.com

10. Skimlinks.com
Tovuti inaitwa skimlinks pia mfumo wao wa matangazo ni katika hali ya maandishi yaani Text Ads kiwango chao cha chini cha kukulipa ni dola 10, Kujiunga Tembelea www.skimlinks.com

Neno la Mwandishi
Ndugu msomaji wetu kumbuka kila kitu ni juhudi na nia kuandika hizo dola ni rahisi, lakini sio Rahisi kuzitia mikononi mwako bila kufanya juhudi katika utafutaji wa watembeleaji katika tovuti, ili upate pesa ya kutosha ni lazima ufanye juhudi, Nikutakie utafutaji mwema.

Imeandika na Riyadi Bhai Swahilitechi.net
Axact

Ibrahim Riyad Houmud

As Salaam Aleikum, I'm Ibrahim Riyadi Houmud, Founder and CEO of RiyadiBhai blog from Mororgoro, Tanzania. I started this blog as a Passion and it now empowering thousands of readers around the globe.Here I usually share news, Adsense tips, wordpress, gadget, widget, Themes, windows, etc.

Post A Comment:

0 comments:

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa