INSTA YAONGEZA KIPENGELE CHA MAGROUP KWAAJILI YA WANACHUO KATIKA APP YAKE

Mtandao wa instagram umekuwa ukifanya maboresho kila siku, hivi karibuni tulisikia kuhusu instagram kuleta sehemu ambayo itakusaidia kutuma picha zinazo potea baada ya muda fulani. Sehemu hiyo kwa sasa ipo kwenye app zote za instagram na unaweza kutumia sehemu hiyo sasa.
Lakini kama haitoshi, hivi karibuni mtandao huo umeanza kufanya majaribio ya sehemu mpya ya magroup ambayo yatakuwa maalum kwaajili ya vyuo mbalimbali. Kwa mujibu wa ripoti kutoka mtandao wa CNBC, Sehemu hiyo mpya itakuwa ikiwaletea taarifa wanachuo mbalimbali kuweza kujiunga na magroup ya vyuo ambavyo wanasoma kwaajili ya kuchat na wanachuo wenyewe kwa wenyewe ndani ya magroup hayo.
Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao huo, vigezo vya mtu kuweza kutumiwa ujumbe wa kujiunga na group la chuo husika bado havija julikana rasmi ila inasemekana kuwa instagram inatazama vitu kama vile, akaunti za chuo unazozifuata, watu unao wafuata pamoja na maneno kwenye description au bio kwenye akaunti yako.


Hata hivyo baada ya kuweza kuletewa ujumbe huo wa kujiunga utaweza kuweka mwaka unaotarajia kumaliza chuo, pamoja na jina la chuo chako na moja kwa moja utaweza kuunganishwa kwenye group ambalo linaendana na chuo na mwaka uliojaza.
Ndani ya group hilo la chuo utaweza kutuma meseji za direct (DM) kwa wanachuo mbalimbali pia utaweza kuona stories za wanachuo moja kwa moja kupitia group hilo.
Kwa sasa sehemu hiyo bado ipo kwenye hatu ya majaribio na inasemekana kuwa, wakati mmoja wa wanahabari wa CNBC waliweza kujiunga na group la chuo japokuwa alikuwa amesha maliza chuo kwa muda mrefu. Kupitia tovuti ya The Verge, Instagram imesema kwa sasa bado sehemu hiyo mpya iko kwenye majaribio ya awali na hivyo ni lazima itakuwa na matatizo mbalimbali.
Bado hakuna taarifa kuhusu sehemu hii kujaribiwa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha zaidi kuhusu ujio wa sehemu hii mpya.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa