JINSI YA KUWEKA CUSTOM RECOVERY KWENYE SAMSUNG GALAXY J7

Samsung Galaxy J7 (SM-J700F) ni moja ya simu zenye uwezo mkubwa licha ya kuwa bei nafuu. Kitu kingine kizuri kuhusu hii simu ni kwamba ina kuja na android 6 (marshmallow) na pia unaweza kutumia SIM card mbili kwa wakati mmoja. Leo tutaona jinsi ya kuweka custom recovery kwenye Samsung Galaxy J7 (SM-J700F)
Custom Recovery ni jambo la muhimu sanaa hasa pale unapotaka kuweka custom rom. Kwa wale wanaopendelea kuweka custom rom kwenye simu zao basi lazima watakuwa wanafahau umuhimu wa custom recovery.

Vigezo na Masharti

  • 0: Mimi sitahusika endapo utaaribu simu yako
  • 1: Hakikisha simu yako ni Samsung Galaxy J7 (SM-J700F)
  • 2: Hakikisha simu yako inatumia android 6.0.1(marshmallow)
  • 3: Soma maelekezo kwa umakini kisha ndio ujaribu kwenye simu yako
  • 4: Hakikisha ume install samsung drivers kwenye computer yako.

STEP 1

Download ODIN program kwa kutumia link chini kisha tengeneza folder kwenye desktop yako. Liweke hilo file ulilo download ndani ya folder kisha lifungue au extract
http://dl.sammobile.com/Odin3_v3.10.7.zip

STEP 2

Download TWRP Recovery kwa kutumia link chini kisha liweke hilo file kwenye folder ulilo tengeneza kwenye STEP 1
https://dl.twrp.me/j7elte/twrp-3.0.2-0-j7elte.img.tar

STEP 3

Kwenye simu yako nenda kwenye settings kisha tafuta kipengele kinachosema Developer Options kama picha inavyo onekana chini. Kama hicho kipengele haukioni basi nenda kwenye about phone kisha shuka chini mpaka utakapoona kipengele kinachosema build number kisha kibonyeze haraka haraka kama mara saba kisha rudi tena kwenye setting na uangalie kama developer options imetokea

STEP 4

Fungua developer options kisha hakikisha umeiwasha (turn on) halafu umeweka tick ua umekiwasha kipengele kinachosema USB debugging kama picha inavyo onekana chini.

STEP 5

Ukiwa hapo hapo kwenye Developer option, hakikisha kipengele kinachosema OEM UNLOCK kipo on kama picha chini

STEP 6

Zima simu yako kisha iwashe kwenye downloading mode. Kama hujui jinsi ya kuwasha simu kwenye downloading mode unachotakiwa kufanya ni zima (turn off) simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kupunguza sauti(vol down button)} na cha kuwashia (power button) mpaka simu itakapowaka kama picha inavyo onekana chini ndipo uachie vitufe vyote kwa pamoja.

STEP 7

Bonyeza kitufe cha kuongeza sauti kwenda kwenye Download Mode na utapata muonekano kama picha chini. Kwa wale watoto wa mama wenye wasiwasi kwamba simu zao zita haribika au unaogopa na unataka simu yako irudi kama kawaida basi toa battery kisha rudishia washa simu yako. Kama wewe hugopi na unataka kuendelea basi endelea kufwatilizia maelekezo



NOTE
Kabla hujaendelea hakikisha kwenye simu yako sehemu iliyoandikwa Product Name ni SM-J700F. Kama ni tofauti na hivyo tafadhali nakuomba usiendelee maana utaaribu simu yako.

STEP 8

Rudi ndani ya lile folder ulilotengeneza kwenye Step 1, kisha double click ile program inayoitwa odin ambayo ulipata baada ya ku extract file ulilo download kwenye STEP 1. Endapo upo sahihi utapata muonekano kama picha chini kwenye computer yako

STEP 9

Chukua USB kisha chomeka kwenye simu yako ya Galaxy J5 (SM-J700F) halafu chomeka kwenye computer kisha kwenye program ya odin utaona kibox kinarangi kimeandikwa com(xx) na neno linalosema added kama picha chini

STEP 10

Kwenye program yako ya Odin bonyeza kipengele kinachosema Ap ambacho kipo kulia kisha utaona window mpya imefunguka. Kwa kutumia hiyo window iliyofunguka chagua lile file ulilo download kwenye STEP 2 ambalo linaitwa twrp-3.0.2-0-j7elte.img.tar kisha bonyeza open. Endapo utafanikiwa basi program yako ya odin itafanana na kama yangu kwenye picha chini.

STEP 11

Chini kwenye program yako ya Odin, bonyeza kipengele kinachosema Start kisha subiri mpaka utakapona program yako ya Odin imesema neno Pass na ina muoenakano kama picha chini. Kisha simu yako itazima na kujiwasha yenyewe.

STEP 12

Simu yako itazima na kujiwasha. Chomoa USB yako kutoka kwenye computer. Utakuwa umefanikiwa kuweka custom recovery kwenye simu yako. Kujua kama umefanikiwa kuweka custom recovery unachotakiwa kufanya ni kuzima simu yako kisha shikilia kwa pamoja vitufe vitatu {cha katikati(home button), cha kuongeza sauti(vol up button)} na cha kuwashia (power button) kwa muda wa sekunde kama tatu au nne kisha achia. Baada ya hapo utaona custom recovery yenye muonekano kama picha chini.



Mpaka hapo tumefikia mwisho. , kama unataka kusaidiwa ku update Samsung Galaxy J7 au simu yoyote unaweza kutucheck kwenye kupitia whatsapp namba +255652732383.Can't talk, whatsapp only.

0 Comments

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa