JINSI YA KUINGIZA PESA KUPITIA YOUTUBE, VIGEZO NA MASHARTI YAKE

As salaam aleikum leo tuangazie jinsi ya kuingiza pesa kupitia youtube hapa nitakujuza vigezo na masharti ya kuzingatia ili kuepuka kufungiwa


1. VIGEZO NA MASHARTI YA KUZINGATIA

  • lazima channel yako ya youtube uwe umeifungua/umeitumia miezi mitatu
  • lazima channel yako iwe na views wasiopungua 10000+
  • Lazima channel yako iwe umei verify (kwa kutumia simu)
  • lazima channel yako iwe na wafuatiliaji (subscribes) 100 kwasasa ila zamani ilikuwa 1000
  • lazima uwe raia wa nchi zinazokubaliwa na youtube kupokea malipo yako
  • la mwisho ni muhimu kuwa na akaunti ya adsense.

2. JINSI YA KUJIUNGA NA MATANGAZO YA YOUTUBE

Haya tuanze kwanza leo niwaombe radhi kuwa sitaweka picha kuhusu maelezo nitakayoyatoa so nisameheane kwa hilo

ingia katika youtube yako kisha bonyeza my channel kisha bonyeza setting kisha bonyeza Advance setting kisha weka alama ya tiki kwenye eneo liloandikwa advertisements kisha upande wa kushoto bonyeza Status and features
kisha bonyeza enable kwenye monetisation baada ya hapo utaona wanakwambia lazima uwe na views wasiopungia 10000 kisha watakwambia usome sheria zao kisha utaambiwa ufungue akaunti ya adsense, utaambiwa uset matangazo unayohitaji yaonekane ukishasoma hayo yote bonyeza sehemu iliyoandikwa Start

weka tiki sehemu zote tatu kuonyesha kuwa umekubaliana na masharti yao kisha bonyeza Accept

kila katika kipengele utaona neno start utabonyeza hapo kila utakapokamilisha kipengele kimoja kisha ukimaliza wataingalia ndani ya masaa nane

kama umekidhi masharti yako utaweza kuanza kuingiza kipato kupitia channel yako ya youtube

Maneno ya muandishi
Imeandikwa na Riyadi Bhai, picha zote kutoka mtandaoni sambaza kama ilivyo kama kuna eneo hujaelewa niachie maswali yako hapo kwenye sanduku la maoni nami nitashughulikia

4 Comments

  1. Habari za kazi samahani nilitaka kufungua Chanel niliiacha kwenye settings sikuletewa ayo maelezo nilikosea nini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sijakuelewa vema kaka naomba urudie swali lako kama itawezekana

      Delete
  2. Jinsi ya kupokea malipo ni kwa njia gani wanayoitumia youtube

    ReplyDelete
    Replies
    1. Salaam!? Mkuu kwanza tufahami kuwa youtube ni tawi la google ivo malipo yake yote yatafanywa na google kupitia akaunti yako ya adsense, katika adsense kuna njia tatu za upokeaji wa pesa zako kwa njia ya bank, cheki na western union. Kujua zaidi kuhusu kupokea pesa zako kutoka adsense soma hapa http://www.swahilitech.net/2017/11/jinsi-ya-kupokea-pesa-zako-kutoka.html ahsante kwa kutembelea mtandao huu washirikishe na marafiki

      Delete

Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa