Twitter hapo jana siku ya Alhamisi imesema kuwa imeondoa akaunti 3,465 zinazofanya kazi kama “operesheni za habari zinazoungwa mkono na serikali” ambazo ilizihusisha na nchi sita: Uchina, Mexico, Urusi, Tanzania, Uganda na Venezuela.
Nchini Uganda, Twitter iliondoa mtandao wa akaunti 418 “zilizokuwa zikishiriki katika shughuli zisizo halali” za kumuunga mkono Rais Yoweri Museveni na chama chake, National Resistance Movement.
Takriban akaunti 268 pia zilifungwa nchini Tanzania baada ya kupatikana kuwasilisha ripoti za nia mbaya kwenye Twitter.
Mexico – 276 akaunti
China – 2,160 akaunti
Urusi – 66 akaunti
Tanzania – 268 akaunti
Uganda – 418 akaunti
Venezuela – 277 akaunti
wasiliana nami
0 Comments
Je unamaoni kuhusu makala uliyoisoma dondosha maoni yako hapa