Articles by "Tricks"
Showing posts with label Tricks. Show all posts
As salaam aleikum ndugu msomaji wa ukumbi huu bila shaka kama wewe ni mtumiaji wa computer utakuwa ushawahi kukutana na hadha kama hii ya kutaka software fulani lakini hauna pesa hivyo ukaamua kuingia google lakini ukaishia kukutana na Trial version
Basi leo nikupe ujanja wa kumalizana na issue hiyo Njia moja unaweza kulikwepa hili ni kuacha kusearch free software kwenye google na badala yake search open source

Mfano kama unahitaji internet downloader manager


Usitafute “Free internet downloader manager” kwenye google search, na badala yake tafuta  “Open source Internet downloader manager”.

hapo utakutana na kile unachokitaka hii ni njia rahisi sana je unanjia nyingine unayoijua funguka nasi katika sanduku la maoni


Njia gani wewe unatumia kupata free softwares?
As salaam aleikum wapendwa baada ya kupotea kutokana na maswala ya kujitafutia mkate wa siku leo nimerudi tena kwaajili yako karibu sana katika blog inayojaribu kukutatulia mambo yako ya kiteknolojia kwa mapana zaidi leo tugusie suala zima la kuwepesisha kupakua file za torent kwa speed kubwa zaidi kwa kutumia IDM yaani Internet Download Manager 

Watu wengi wamekuwa wakitumia torrent clients ( kama u-torrent, bittorrent, vuze etc) kwa ajili ya kupakua movies na apps zenye file kubwa kutoka kwenye torrents sites mbalimbali lakini huwa kunakua na changamoto ya speed kuwa ndogo unapokua unapakua file hasa lenye seeders wachache ....ili kuepukana na changamoto hyo leo ntakujuza njia ya kupakua files kwa kasi zaidi;

1. kwanza kabisa  unatakiwa uwe na internet download manager (IDM) kama hauna download hapa bure kabisa DOWNLOAD

2. Link internet download manager na browser unayotumia mimi huwa natumia chrome unaweza kupakua chrome browser hapa DOWNLOAD

3.Unatakiwa ufungue account kwenye website inayoitwa www.seedr.cc ambako utapewa disk kama 2gb ( ila inaweza kufikia 5GB ukifanya sharing na rafiki zako kupitia referral code yako) 4.Ukishafungua hiyo account utakwenda kwenye torrent site unayopendelea either rarbg.to , katcr.co , limetorrent.cc 13377x.to etc5 . Copy magnet link ya file kama unavyoona katika picha hapo juu unalotaka kudownload na paste kwenye seedr.cc 


account kuna sehemu imeandikwa paste, kisha bofya kitufe cha jumlisha 

na file lako litaundwa na utaona mshale wa kupakua ukiweka mouse yako katika folder lililoundwa angalia picha hapa chini
na utaweza download kwa kasi nzuri sana ambayo ni tofauti kabisa kama ungetumia utorent

asante kwa kusoma makala hii sambaza upendo kwa washkaji kwa kushare makala hii karibu tena
As salaam aleikum ndugu zangu kila kukicha mambo yanabadilika na Tech inakuwa au inazidi kutanuka kila siku zinavyosonga wenda unatamani kufahamu na kutumia vitu vingi ila gharama imekuwa ni changamoto yako kubwa leo tutumie express VPN bure bila malipo hata ndururu, kwanza tufahamu VPN ni kiumbe gani katika anga za Tech

1.VPN.
Visual private network (vpn) hii kama inavyojieleza ni private network ambayo inakusaidia wewe kutembelea tovuti mbali mbali bila kuweza kuonyesha address yako wala location uliyopo hii inakuongezea wewe security kwa kuwa wadukizi wengi(hackers) huwa wanatumia ip address yako ili kuweza kukudukua lakini vpn huwa inatumia technology inayojulikana kama TUNNELING ilikuweza kuficha address yako hivyo kuwa vigumu kwa wewe kuweza kudukuliwa 

MATUMIZI YA VPN.
-watu wengi hutumia vpn ili kuweza ķuingia kwenye websites ambazo huwa zinatumika kwenye nchi husika na kwenye nchi nyengine haipatikani yaani ukiingia either ikuandikie website not available au isifunguke kabisa mfano labda unakuta tovuti inatumika marekani tu au urusi tu na nchi nyengine wameblock unaweza kutumia vpn kufake ip adress yako ikaonekama kama upo kwenye hiyo nchi na uka access hiyo tovuti watu wengi hutumia hii njia hasa wale walioko nje huko mfano china.

-pia wengi hutumia vpn katika apps(hapa namanisha hata zile apps za games pia) ambazo zimezuilika kutumika nje ya mipaka ya nchi husika mfano kuna hii apo inaitwa SPOTIFY hii app sana sama inatumika marekani na nchi nyengine za ulaya ila kwa huku kwetu kuitumia mpaka vpn ni app ambayo inakuruhusu wewe kuweza kutengeneza online playlist yako ya miziki ambayo utaweza kuisikiliza kwa muda uutakao bila kuweza kujaza storage yako ya simu hivyo kufungua account kwenye hii app itakubidi utumie vpn kupata ip address ya hizo nchi ambayo ipo active.

AINA ZA VPN.
vpn huja kwa aina mbili kuu mfano ni hizi
-built in device vpn (hizi huwa zipo katika software ya simu au laptop yako).
-downloadable vpn hizi zipo apps zake ambazo kampuni inayomiliki ndiyo inakupa ip address kwa malipo.
sisi tutaizungumzia hiyo ya pii hapo.

DOWNLOADABLE VPN/VPN APPS.
Kama nilivyosema hizi ni zile vpn ambazo itakubidi u download app husika ili kuweza kuzitumia app hizo mfano ni hii EXPRESS VPN app hii ina jina kubwa na pia ina watumiaji wengii sana duniani na ina feature nzuri pia ipo effective na simple kutumia hivyo mada ya leo itahusu namna ya kuidukua ili upate matumizi ya mwaka mzima bureee ndio nikisema bure namaanisha hautalipia hata kumi ila itabidi ufuate maelekezo haya kwa umakini.

EXPRESS VPN.
hii app kama nilivyoelezea hapo juu ni nzuri mno ila ukii download itakuhitaji uweke email yako ili uweze kujisajili na kupata siku saba za bure kisha baada ya hapo utalipia ili kuweza kutumia (kitu ambacho ni gharama).

NAMNA YA KUDUKUA.
Fuata maelezo haya hapa chini.

1).Ingia playstore kisha download app hii inayoitwa express vpn kisha wacha iji install.


2).Baada ya kui install ifungue kisha itakuletea option mbili ambazo ni sign in na start free trial basi baada ya hapo usiguse chochote bali toka nje ya hiyo app yaani gusa home button urudi kwenye home menu ya simu.


3).kisha baada ya hapo ingia google kisha andika hivi
(Tempmail) kisha search itakuleta kwenye link mbali mbali chagua hiyo ya kwanza ipo hivi (http//temp-mail.org) kisha iguse.


4).itafunguka kisha hapo kwenye homepage ya hiyo tovuti utaona kuna email sasa hapo wewe i hold kisha i copy hiyo email kisha rudi kule kwenye ile express vpn app yako.


5).basi baada ya kurudi kwenye express vpn gusa hapo kwenye start free trial itakuleta kwenye page nyengine ambayo utaona kuna sehemu ya kujaza email na imekuandikia hivi (try express vpn free for 7 days ) hap kwa chini kwenye hilo box/kijisanduku hold kisha paste hiyo email 
Note ;kama umeshindwa ku copy na kupaste kwenye simu direct basi andika pembeni hiyo email either kwa kalamu kisha utaiandika kama ilivyo kwenye kijisanduku kile .


6).baada ya hapo gusa hapo kwenye start free trial kisha wacha iji load basi hapo utakuwa umeshamaliza kui dukua(bali si terminology inayoendana).


Ukiangalia hapo juu utaona umepewa siku 299 au zaidi za kutumia free .
Sasa hapo ni wewe kuchagua nchi unayopendelea kisha start vpn anza kuzama mitandao unayotaka hapo upo safe kabisa .


Na pia unaweza ukatumia hii vpn ukichanganya na deepweb browsers mfano orbot na orfox au onion browser yoyote hii itakufanya usiwe tracked.


N.b
Pia kama hizo siku zikiisha unaweza kuifuta kisha ukadownload nyengine halafu ukarudia procedure kisha maisha yakaendelea.


Credit: JamiiForums
As salaam aleikum ndugu msomaji, umeamka asubuhi na mapema unawahi kibaruani kwa ajiri ya kufanya presentation (mrejesho), shingoni au mfukoni umeweka flash yako yenye presentation nzima unayotakiwa kufanya siku hiyo, barabarani foleni inakuchelewesha unafika ofisini katika ukumbi wa mikutano unakuta watu wamenuna kwa kukusubiri. Unajaribu kuomba msamaha na watu wanakuelewa, ile kuchomeka flashi katika kompyuta yako unashtushwa na unachokiona, mafile yote hayaonekani. Hapo unaanza kuchanganyikiwa na kuanza kufikiria jinsi ya kuomba msamaha kwa mara ya pili huku wasiwasi ukikushika juu ya hatma ya kibarua chako.

Ondoa shaka, unaweza ukarudisha mafile yako yaliyojificha bila tabu na kuendelea na presentation yako. Kitu cha muhimu kufahamu ni kwanini mafile yako yamejificha?

Sababu zinazosababisha kujificha kwa mafile katika USB Flash drive yako

  • Virusi vya kompyuta
  • Settings za kompyuta yako
  • Hitilafu katika Flash


Kuna njia tofauti za kurudisha mafile yaliyofijicha kutegemea na sababu iliyosababisha kujificha kwa mafile hayo

Njia ya Kwanza: Hapa inategemea na toleo la mfumo endeshi unalotumia, kwa watumiaji wa Windows 8, 8.1 na 10 fungua This Pc au My Computer, na angalia katika ribon ya juu ( Menu bar), chagua view–>tiki sehemu iliyoandikwa Hidden Items na hapo mafaili au mafolder yaliyojificha yataonekana.Njia ya Pili: Hii ni kwale ambao mafile au mafolder yao yamefichwa na virus, hapa tutamia cmd ili kuweza kurudisha mafile yetu yaiyojificha.

Fungua Command Prompt kwa kubonyeza alama ya Windows + X kwa pamoja, shusha mpaka kwenye Command Prompt ili kufungua. Au unaweza ukafungua start menu kwa watumiaji wa Windows 7, fungua run alafu andika cmd kisha bonyeza enter ili kufungua.

Hapa tufanye pendrive (flash) yako imepewa herufi G: kwenye windows explorer, alafu andika komandi zifuatazo au Copy na Kupaste komandi hizi kwa right click kwenye cmd na kupaste,

attrib -h -r -s /s /d g:\*.*


Badilisha herufi g: kuwa herufi za flash yako. Alafu bonyeza enter , utaona mstari huo wa maandishi unarukia katika mstari wa pili. Hapo mafile yako yote yaliyojificha yataonekana yote hata kama yalikuwa yamefichwa na virus.

Njia ya Tatu: Tumia Antivirus program unayoiamini kama Kaspersky au Norton kuscan Flash yako au unaweza ukadownload tool itakayokusaidia kuondoa virus aina ya Autorun hapa. http://ccm.net/download/download-11613-autorun-exterminator . Kisha install, hii itakusaidia kuondoa autorun.inf wote waliopo kwenye kompyuta yako pamoja na kwenye flash drive yako.

Zingatio: Hakikisha una install Antivirus Program ya kuaminika katika kompyuta yako au update antivirus iliyopo ili kukuongezea usalama.
As salaam aleikum ndugu msomaji wetu, bila shaka Mara kadhaa tumekuwa tukishindwa kuhamisha mafaili kama picha, video au miziki kutoka katika kompyuta zetu kwenda kwenye smartphones kwa sababu tu ya kukosa USB Cable.


Fikiria umetoka nyumbani na upo ugenini au mgahawani, kuna nyimbo au video moja unayoipenda sana unaiona katika kompyuta ya rafiki yako na unatamani sana uwe nayo kwa muda huo. Ukamuomba rafiki yako akupatie, bila kinyongo akakuruhusu kuichukua, unaanza kuingia kwenye mfuko au mkoba wako kutafuta USB Cable yako ili uweze kuihamisha na unagundua USB uliiacha nyumbani. Unaanza kukosa raha kwa sababu kitu ukipendacho unakikosa kwa sababu ya cable tu.

Ondoa shaka, hapa ndipo ES File Explorer inapoingia. Es File Explorer ni application inayokuwezesha kumanage mafaili yako yote yawe ya katika simu yako, katika kompyuta yako au katika huduma za kuhifadhi data za kimtandao (Cloud Storage).

ES File Explorer ni application ya muhimu zaidi kuwa nayo katika simu yako kama wewe ni mtumiaji wa smartphone. Hebu tuangalie vitu ambavyo ES File Explorer inaweza kukusaidia wewe kama mtumiaji wa Smartphones zinazotumia mfumo endeshi wa Android.

Kuhamisha mafaili kutoka katika kifaa kimoja kwenda kingine kwa kutumia network (mtandao)
Kumanage mafaili ya simu yako yote kwa kutumia Application moja, kama kubadili majina ya mafaili.
Inakuwezesha kucopy na kupaste mafaili mengi kwa wakati mmoja
Inakuwezesha kutafuta (search) faili lolote katika simu yako bila tabu kwa kuandika tu jina la faili
Inakuwezesha kubadilisha muonekano wa mafolder yako, kama kuyapanga katika mpangilio mzuri zaidi.

Inakuwezesha kuyazip mafaili yako (kuyabana na kuyapunguza ukubwa) ili kuweza kuyatuma kwenye barua pepe kirahisi.
Kuangalia video au kusikiliza mziki kutoka kwenye kompyuta yako bila kuzisave kwenye simu yako (streaming)
Kulinda mafaili yako ya muhimu kwa password.

Jinsi ya kuhamisha mafaili kutoka katika kompyuta kwa kutumia ES File Explorer
Pakua (download) ES File Explorer kwenye simu yako kutoka Google Play Store au unaweza ukatumia linki hii ES File Explorer

-Install hiyo Application katika simu yako

-Washa WiFi Hotspot katika simu yako ili kuweza kupata network itakayounganisha simu yako pamoja na kompyuta yako, fanya hivyo kwa kwenda kwenye Settings–>More–>Tethering & portable hotspot–>Wi-Fi hotspot. Washa hapo alafu fungua sehemu hiyo hiyo ili kuset jina na password utakayotumia katika Wi-Fi yako.


-Nenda kwenye kompyuta yako na unganisha Wi-Fi inayorushwa na simu yako kwa kuingiza password ileile uliyoiweka kwenye Wi-Fi hotspot.

-Baada ya kompyuta yako kuunganishwa na Wi-Fi, nenda kwenye folder au File unalotaka kulihamisha, right click na nenda mpaka kwenye Properties, mara nyingi inakuwa chini kabisa.

-Baada ya properties kufunguka, nenda kwenye sharing alafu bonyeza share, everyone ili isikupe shida baadae. Ukimaliza funga hilo file.

-Baada ya hapo nenda kwenye simu yako kisha fungua ES File Explorer

-Bonyeza alama ya menu upande wa kulia juu ya application yako, kisha nenda mpaka kwenye network–>LAN

-Baada ya LAN kufunguka, bonyeza alama kama ya duara hivi kwa juu ili uweze kusearch vifaa vilivyopo karibu na wewe vinavyotumia network moja. subiri kwa muda, ikimaliza utaliona jina la kompyuta yako au ya rafiki yako katika application yako.


-Bonyeza hilo jina ili uweze kuifungua, itakuletea sehemu ya kuingiza username na password ya hiyo kompyuta’ utaingiza username na password za ile kompyuta.

-Baada ya hapo utaweza kuona mafaili yote uliyoyaruhusu kwenye sharing na utaweza kuyahamisha bila tabu kwa kuyabonyeza tu.

Kumbuka: Unaweza ukatumia Wi-Fi ya ofisini, nyumbani au shuleni kuhamisha mafaili bila kutumia Wi-Fi Hotspot ya simu yako. Ila ni vyema kutumia Wi-Fi Hotspot ili kuongeza usalama wa mafaili yako na kasi ya kuhamisha. Sio lazima uwe na kifurushi cha data kufanya hivi.

Tutakuletea makala maalumu  ya ES Explorer ili uweze kuielewa zaidi application hii katika makala zinazokuja, usikose kutembelea tovuti hii ili kuweza kupata maujanja zaidi.
As salaam aleikum ndugu mfuatiliaji wa blog hii, Leo nimeamua kushare na nyinyi mkeka wa komandi za Linux ili iwe rahisi kudhibiti baadhi ya mienendo ya mfumo wako au kufanya baadhi ya kazi kwa wepesi zaidi kama wewe ni mtumiaji wa linux au ni System Admin.

Kama upo tayari kuwa msimamia mifumo ya kompyuta inayoendeshwa na mfumo endeshi wa Linux ni vizuri kujifunza komandi muhimu za kuendesha au kufanya mambo ya msingi kwa haraka. Hapa ni lazima uwe na mkeka mwepesi ulijaa komandi zote za msingi ili kufanya yote hayo, usisahau kuprint ili uwe nao karibu muda wote kwa sababu ni ngumu kidogo kukumbuka mkeka wote.

Unaweza ukapata mkeka huu katika mtindo wa pdf kwa kubonyeza hapa.
Android Device Manager itakuwezesha kuiloki simu yako iliyopotea, kuipiga na ikaita kwa nguvu hata kama ilikuwa kwenye silent mode, kufuta data zilizokuwemo pamoja na kuonyesha eneo ilipo kama bado haijazima.

Sio mara zote huwa tunakumbuka sehemu tulipoweka simu zetu na hii huwa inatoa changamoto sana kwetu. Fikiria umeamka asubuhi na umeshajiandaa tayari kwa kwenda kibaruani, unatafuta simu bila mafanikio na muda unazidi kwenda. Hofo ya kuchelewa kazini inaongezeka hasa katika kipindi hichi cha hapa kazi tu na unajikuta umechanganyikiwa kabisa.
Kitu kikubwa tunachofanya katika mazingira kama haya huwa tunajaribu kujipigia labda inaweza ikaita na ukajua ulipoiweka. Sasa je, kama simu yako ilikuwa katika silent mode wakati unalala unadhani utafanyaje?
Hapa ni rahisi tu, watengenezaji wa mfumo wa android waliliwaza hili na kuamua kuleta mfumo maalumu wa kusaidia watu waliopoteza simu zao. Huduma hii inafahamika kama Android Device Manager ambayo itakuwezesha kupiga simu yako na ikaita hata kama ilikuwa kwenye silent mode, kuiloki ukiwa mbali, kufuta data zilizokuwemo kwenye simu yako pamoja na kuonyesha eneo ilipo kama ilikuwa bado haijazimika. 

Njia za kufuata ili kutafuta simu yako iliyopotea;

  • Tembelea Android Device Manager ya Google kwa kutumia kompyuta yako kwa kugonga hapa
  • Ingia kwa kuweka taarifa zako za Gmail kama zile ulizotumia katika simu yako na Google play. Hapa namaanisha Email yako na Password.
  • Baada ya kuingia utaona vitu vinne, Jina la Simu yako na tarehe ya mwisho kuingia, na option (machaguo) nyingine za Ring, Lock na Erase.
  • Ukibonyeza option (chaguo) la Ring simu yako itaita kwa sauti kubwa sana hata kama uliiweka katika silent mode, hii itakusaidia kuipata kiurahisi kama umesahau mahali ulipoiweka.
  • Pia unaweza ukailoki kwa kubonyeza chaguo la Lock, hapa simu utaletewa ukurasa wa kuingiza maneno amabyo utataka yatokee kwenye simu yako, unaweza ukaingiza namba yako ya simu pamoja na maneno kama “Tafadhali irudishe simu kwa mmiliki wake au piga namba hizo”.
  • Kama unahisi simu yako ilikuwa na taarifa za muhimu sana basi chaguo la ERASE ndio mahali pake, hii itafuta kila kitu kilichomo kwenye simu na kuokoa data zako zisianguke mikononi mwa watu.
  • Pia kuna sehemu ya kuonyesha eneo ilipo kwa kutumia ramani kubwa inayoonekana katika kioo cha kompyuta yako kwa wakati huo.
Pia kwa sasa Google wameleta njia rahisi tu ya kutafuta simu yako kwa kuandika Lost Phone katika ukurasa wao wa kutafuta na kama umelogin kwenye akaunti yako google watakuletea ramani ya eneo ilipo simu yako.
Unapoamua kuiloki simu yako kupitia huduma hii tafadhali usisahau Password yako.