Articles by "News"
Showing posts with label News. Show all posts
As salaam aleikum Yawezekana umewahi kusikia kuhusu teknolojia ya Wi-Fi na pengine na wewe ni miongoni mwa wanaotumia teknolojia hii. Kama hujui, hii ni teknolojia inayokuwezesha kupata intaneti kwenye simu yako ya mkononi, tablet, kompyuta au vifaa vingine vyote vinavyotumia intaneti.

Kwa kutumia Wi-Fi, unaweza kutazama video mtandaoni, unaweza kusikiliza muziki, kuingia kwenye mitandao ya kijamii, Instagram, Facebook, WhatsApp, Snapchat na mitandao mingine kibao. Kwa kifupi, unaweza kufanya kila kitu kinachohusianana intaneti bila kuwasha ‘data’ kwenye simu yako.

Unachotakiwa ni kuwa tu sehemu yenye Wi-Fi, kisha unaji-connect kwa kupitia simu yako au kifaa chochote kinachotumia intaneti na unaendelea kuperuzi kwenye mitandao kwa kasi kubwa pengine kuliko ukitumia ‘data’, kutegemea na uimara wa Wi-Fi mahali ulipo.

Wakati Wabongo wengi ndiyo kwanza wameanza kuishtukia teknolojia hii na kuanza kuitumia kwa kasi, kwenye maofisi mengi kukiwa kumefungwa vifaa maalum vya kukuwezesha kupata Wi-Fi bila chenga, nchi za wenzetu tayari kilishakuwa kitu cha kawaida sana na yapo baadhi ya majiji ambayo unapata Wi-Fi ya bure popote ulipo!

Kwa jinsi dunia inavyokwenda kasi, wakati sisi ‘tukihangaika’ na Wi-Fi, tayari wanasayansi kwenye nchi zilizoendelea, wamegundua teknolojia mpya, yenye kasi ya zaidi ya mara mia moja ya Wi-Fi ya kawaida.

Teknolojia hii inaitwa Li-Fi (Light Fidelity) na tofauti na Wi-Fi inayotumia mawimbi ya radio (radio waves), Li-Fi inatumia mawimbi ya mwanga (Light Waves).

Kinachofanyika ni kwamba, taa maalum (LED Light) ndizo zinazotumika kusambaza mawimbi ya Li-Fi na watu waliopo ndani ya eneo ambalo mwanga wa taa hiyo unafika, wanakuwa na uwezo wa kupata intaneti yenye kasi kama ya mwanga! Yaani hata kama video ni kubwa kiasi gani, ukitaka kudownload, unagusa tu na ndani ya sekunde chache kazi inakuwa imeshakwisha.

Taa hizo huwa zinaunganishwa na kifaa maalum ambacho ndicho kinachopokea intaneti kutoka kwenye satelite, kisha kinaibadilisha kwenda kwenye mawimbi ya mwanga na kuisambaza kupitia taa hizo, ambazo zinatakiwa kuwashwa muda wote ili kupata intaneti. 
Kasi ya Li-Fi, ni 224 gigabits/seconds na kama nilivyokueleza, ni zaidi ya mara 100 ya Wi-Fi ya kawaida. Mgunduzi wa teknolojia hii ni Profesa Harald Haas wa Chuo Kikuu cha Edinburgh nchini Uingereza na tayari imeshafanyiwa majaribio nchini Uingereza, Marekani, Dubai na maeneo mengine duniani.

Changamoto kubwa ni kwamba, ili kuwahudumia watu wengi zaidi, taa zinatakiwa kuwa nyingi na zinatakiwa kuwashwa muda wote, hata mchana. Pia Li-Fi haina uwezo wa kuvuka ukuta, taa ikiwashwa ni wale tu waliopo ndani ya eneo mwanga unapofika ndiyo watakaopata intaneti.

Ili kukabiliana na tishio la Li-Fi inayoonekana kama itakuja kuliua soko la Wi-Fi, Kampuni inayotoa huduma za Wi-Fi ipo mbioni kuanza kutumia teknolojia mpya iitwayo Wi-Fi HaLow ambayo nayo itakuwa na kasi kubwa zaidi ambayo hata hivyo, bado haitaifikia Li-Fi.

Tayari makampuni makubwa kama PureLiFi, Lucibel, Icade na Phillips pamoja na Jeshi la Marekani yameongeza nguvu na kuanza katika project hiyo kubwa na kuanza kutengeneza vifaa vyenye uwezo wa kupokea mawimbi ya Li-Fi na matarajio ni kwamba mpaka ikifika 2020, Li-Fi itakuwa imesambaa dunia nzima.
Kampuni ya Yahoo ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma za barua pepe, hivi karibuni imetangaza kuja na huduma mpya ambayo itawaruhusu watumiaji wa huduma za Yahoo kuweza kuchat na ndugu na jamaa pamoja na marafiki kwa kutumia huduma mpya inayoitwa Yahoo Together.
Yahoo Together ni app ambayo imechukua muonekano na mtindo wa App ya Slack ambayo pia hutoa huduma ya kuchat kama ilivyo kwenye app hiyo mpya ya Yahoo Together. Tofauti na app ya Slack, App hii mpya ya Yahoo inakupa uwezo wa kuchat kwenye magroup lakini ni lazima kuwa na barua pepe ya mtandao wa Yahoo ndipo uweze kutumia app hiyo mpya.

Moja kati ya sehemu nzuri kwenye app hii ni sehemu inayoitwa Smart Reminders, sehemu hii itakuwezesha kuweka meseji ili ijitume yenyewe kwa wakati fulani na muda huo utakapo fika meseji hiyo itajituma kwa watu wote kwenye group husika. Sehemu nyingine ni Blast, highlights sehemu ambazo zitakupa uwezo wa kuwekea rangi kwenye meseji fulani ili watu wengine kwenye group waweze kuiona meseji husika pale watakapoingia kwenye group.
Kwa sasa tayari app hii ipo kwenye masoko ya Play Store na App Store hivyo unaweza kuipakua moja kwa moja kupitia masoko hayo
Hapo asubuhi ya jana, kampuni ya Facebook kupitia ukurasa wake wa habariilichapisha taarifa juu ya udukuwaji uliofanyika siku za karibuni. Kupitia habari hiyo Facebook imeandika kuwa imegundua tatizo kwenye mtandao huo ambalo limeletwa na mdukuaji au wadukuaji ambapo akaunti zaidi ya milioni 50 zinaweza zikawa zimeadhiriwa.
Kwa mujibu wa Facebook kupitia udukuaji huo ulifanyika kwa kutumia sehemu maalum inayopatikana kwenye App ya Facebook ambayo inajulikana kama “View As”. Kwa wale ambao hamjawahi kutumia sehemu hii, hii ni sehemu inayo kuruhusu kuweza kuangalia ukurasa wako kama mtu mwingine ili kuweza kuona ukurasa wako unaonekanaje pale mtu anapokuwa ana tembelea ukurasa huo.
Sasa kupitia udukuaji uliofanyika Facebook inadai kuwa, wadukuaji au mdukuaji anaehusika alikuwa akitumia sehemu hiyo kuweza kuiba token (ziko kama mfululizo wa namba nyingi) ambazo hizi ndio husaidia mtu anapokuwa ameingia (login) kwenye App ya mtandao huo kuweza kuendelea kutumia mtandao huo bila kuingia (login) kila wakati anapotaka kutumia app hiyo ya Facebook.
Hata hivyo makala hiyo inaendelea kuandika kuwa, kampuni ya Facebook iligundua kuhusu udukuaji huo siku ya tarehe 25 ya mwezi September baada ya kupewa taarifa na Guy Rosen ambaye ni Makamu wa rais wa usimamizi wa bidhaa wa kampuni ya Facebook. Hata hivyo mara baada ya kupewa taarifa na mfanyakazi huyo, Facebook ilichukua hatua ya kuzima sehemu “View As” na baadae kulazimisha watumiaji milioni 90 walio wahi kutumia sehemu hiyo kwa kipindi kirefu kuweza kuingia (Login) upya kwenye akaunti zao na kuwapa ujumbe wenye kuonyesha ni kwanini.
Kwa mujibu wa tovuti ya TheVerge, udukuaji huu unakuja masaa machache kutoka mdukuaji salama “white hat hacker” wa nchini Taiwan Chang Chi-yuan, kutangaza kuwa amegundua tatizo kwenye mtandao wa Facebook tatizo ambalo linamuezesha kuweza kufuta ukurasa wa Facebook wa mkurugenzi mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg. Hata hivyo mdukuaji huyo salama alitanga hayo kupitia kwenye mtandao wa Facebook na kusema kuwa ataonyesha tukio hilo mubashara kupitia ukurasa wake wa Facebook kama kitendo cha kufundisha watu jinsi ya kugundua matatizo kama hayo.
Hata hivyo baadae “white hat hacker” huyo alitangaza kuwa ameamua kuwasilisha tatizo hilo kwa kampuni ya Facebook na hivyo hatoweza kuonyesha mubashara tukio hilo la kifuta ukurasa wa Zuckerberg na kudai kuwa atakuja kuonyesha pale atakapo pewa zawadi ya pesa za kugundua tatizo hilo kwenye mtandao huo. Facebook na makampuni mengine makubwa ya mtandaoni huwa na utaratibu wa kutoa zawadi ya pesa kwa wadukuaji salama “white hat hacker” wakionyesha matatizo mbalimbali ya ulinzi ya mitandao yao.
Kama ilivyo andikwa kwenye ukurasa wake, Facebook hutoa kiasi cha chini cha dollar za marekani $500 ambayo ni sawa na Tsh 1,143,000 kwa tatizo la ulinzi litakalo gundulika na mdukuaji salama na hutoa pesa zaidi ya hizo kulingana na tatizo lilogundulika, yaani ni sawa na kusema tatizo linapokuwa kubwa zaidi basi ndio kiasi cha pesa kinakuwa kikubwa zaidi.
Mdukuaji huyo ChiYuan Chang, anajulikana kwa kazi yake ya udukuaji salama na ameandikwa kwenye ukurasa wa mtandao wa LINE wa mwaka 2016 kama mmoja wa wadukuaji wazuri waliosaidia mtandao huo kugundua matatizo mbalimbali.
Kwa sasa Facebook imeshatoa taarifa kwa mamlaka husika nchini marekani na tayari sehemu hiyo imeshafanyiwa marekebisho ila Facebook inasema kuwa bado haijampata anae husika na udukuaji huo na inawezekana kutokumjua kabisa kutokana na aina ya udukuaji uliofanyika. Vilevile Facebook hivi leo inakabiliwa na kesi ya kujibu iliyofunguliwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao huo wakidai kuwa udukuaji huo wa Facebook umesababisha uwezekano wa watu kuweza kuiba utambulisho wao “identity theft” kwa urahisi zaidi.
RAM ni kiungo cha muhimu sana kwenye simu za mkononi, RAM husaidia simu kufanya kazi kwa haraka na pia husaidia simu kuwa na uwezo wa kufungua programu nyingi kwa wakati mmoja, vilevile RAM ni muhimu kwa wale wapenzi wa kucheza Game kwenye simu kwani hii ndio uchukua nafasi kubwa kwa kukupa uwezo wa kucheza game bila kukwama kwama.
Sasa baada ya kujua umuhimu wa RAM kwenye simu sasa hebu ngoja nikujuze hili, hivi karibuni utanza kuona simu zenye uwezo mkubwa wa RAM kama ilivyo kompyuta. Hayo yamebainika baada ya kampuni ya Oppo kuonekana ikitrajia kuleta simu yake mpya yenye uwezo wa RAM ya GB 10.
Kupitia tovuti ya TENAA ambayo hutumiaka kutoa vibali kwaajili ya simu zote zinazoingia sokoni au zinazotarajia kuingia sokoni nchini China, simu hiyo ambayo ni toleo jipya la simu ya Oppo Find X limeonyeshwa kuja na RAM kati ya GB 10.
Mbali na hayo simu hiyo imeonekana kuja na kila kitu kinacho liangana na toleo la kwanza hivyo ni RAM pekee ndio inayotazamiwa kuongezeka kwenye toleo jipya la simu hiyo.
Kwa sasa bado hakua taarifa zaidi kuhusu lini toleo jipya la simu hii litakuja rasmi hivyo kupata habari zaidi kuhusu simu hii hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Swahili Tech.
Kampuni ya Google ni moja kati ya kampuni kubwa sana kwa sasa, kampuni hii imetoka mbali sana na hapo jana kampuni ya Google imetimiza miaka 20. Kwenye miaka hiyo 20 kampuni ya Google imebadilika sana kutoka kampuni iliyoanzishwa na watu wawili kwaajili ya majaribio, hadi kufikia kampuni yenye thamani ya dollar za marekani bilioni $110.8 ambayo ni sawa na Tsh Trilioni 252.
Kwenye miaka hii ishirini 20 ya Google hebu twende tukaangalie historia ya kampuni hii ilipotoka. Kwa kuanza labda turudi nyuma kidogo hadi mwaka 1996, Mwaka huo wagunduzi kutoka chuo cha Stanford cha nchini marekani Sergey Brin na Larry Page walianza kufanyia kazi project yao ya kwanza ambayo ilikuwa inahusu mambo ya tovuti na jina la project hiyo lilikuwa Backrub.
Backrub ilikuwa ni project ya mtandaoni ambayo ilibuniwa maalum kwaajili ya kutathmini umuhimu wa tovuti au (Domain) kwa kuangalia kiasi cha link (backlink) kwenye domain au tovuti kwa ujumla. Baada ya ubunifu huu Sergey Brin na Larry Page walibadilisha jina la project hiyo na kuwa Google.
Jina Google lilitokana na neno la hisabati ambayo maana yake ni moja (1) na sufuri miamoja (100), kutoka kipindi hicho Google ilipata kujulikana na watu wengi hadi hapo mwaka 1998 ambapo Google ilipata mwekezaji wa kwanza anayeitwa Andy Bechtolsheim ambaye ni mgunduzi wa kampuni ya Sun Microsystems, ambaye yeye aliwekeza dollar za marekani $100,000 ambayo kwa sasa ni sawa na takribani Tsh milioni 230 kwa kipindi hicho lazima ilikuwa ni pungufu ya hapo.
Baada ya kupata pesa hizo waanzilishi hao wa Google, Sergey Brin na Larry Page walianzisha ofisi yao ya kwanza ambayo ilikuwa ni sehemu ya kuhifadhi vitu (Garage) ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Susan Wojcicki ambaye sasa ni mfanyakazi wa Google na mkurugenzi mtendaji wa YouTube.
Kuanzia hapo Google imekuwa kutoka kampuni changa hadi kufikia sasa na ukweli ” ukiona nyani mzee ujue amekwepa mishale mingi ” historia ya Google haijagubikwa na mambo mazuri tu na uhakika yapo mambo mengi sana ambayo yalikuwa yawakatishe tamaa wabunifu wa kampuni hiyo mengine yameandikwa na mengine hayaja andikwa. Kwa mfano kampuni moja inayoitwa Excite ilikataa kununua kampuni ya Google kipindi hicho bado changa lakini sasa loh.. na hakika wanajuta.
Historia ya Google ni fundisho kuwa inawezekana kwa sasa jambo unalo lifanya linaonekana halina dhamani ila na hakika ukiendelea kufanya jambo hilo bila kujali maneno ya watu na bila kukatishwa tamaa na uhakika lazima siku moja utakuja kufanikiwa.
Mtandao wa Instagram ambao kwa sasa unamilikiwa na kampuni ya Facebook ulianzishwa mwaka 2010 na waanzilishi Kevin Systrom na Mike Krieger, toka kipindi hicho mtandao wa Instagram umekuwa kwa kasi hadi kufikia mwaka 2012 ambapo Facebook ililipa dollar za marekani bilioni $1 kwaajili ya kununua mtandao huo.
Baada ya Facebook kununua mtandao huo, mtandao wa Instagram umeendelea kukuwa kwa kasi hadi kufikia kiasi cha watumiaji zaidi ya bilioni 1. Kwa kipindi chote hicho waanzilishi wa mtandao huo Kevin Systrom na Mike Krieger waliendelea kufanyia kazi mtandao huo wa Instagram lakini ikiwa ni chini ya kampuni ya Facebook.
Sasa habari za hivi karibuni kutoka kwenye mitandao mbalimbali zinasema kuwa, waanzilishi wa mtandao wa Instagram Kevin Systrom na Mike Krieger wametangaza kuachana rasmi na mtandao wa Facebook, taarifa hizo zilizuka hapo siku ya jana na kutangazwa rasmi kupitia mtandao wa New York Times. Hata hivyo baadae taarifa hizo zilidhibitshwa kwa taarifa maalum iliyotolewa na mmoja ya waanzilishi hao kupitia mtandao huo.
Kupitia taarifa hiyo iliyotolewa na Kevin Systrom kwenye blog ya habari ya Instagram, Systrom ameandika kuwa “Tunatarajia kuchukua muda mwingi kuchunguza udadisi wetu na ubunifu wetu,” aliandika. “Kujenga mambo mapya inahitaji sisi kurudi nyuma na kuelewa nini kina tuhamasisha na pia kitu hicho kiendane na mahitaji ya dunia; ndio tunachotaka kufanya.” aliandika Systrom muanzilishi mwenza wa mtandao huo wa Instagram.
Hivi karibuni waanzilishi wengine wa programu ya WhatsApp kwa nyakati tofauti waliatangaza kuachana na kampuni ya Facebook, huku mmoja wao akitangaza kuachana na kampuni hiyo mara baada ya kutofautiana na kampuni hiyo juu ya uendeshaji wa mtandao wa Facebook na WhatsApp kwa ujumla kwa kile kilichosemekana kuwa ni kutokuzingati sera za faragha za watumiaji wa programu ya WhatsApp pamoja na Facebook kwa ujumla.
Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti mtendaji na mwanzilishi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg aliandika kwenye maelezo yake kuwa “Nimejifunza mengi kufanya kazi nao kwa kipindi cha miaka sita na nimefurahia sana. Ninawatakia mema wote na ninatarajia kuona kile watakachojenga baadaye. ” alisema Mark baada ya kupokea taarifa ya waanzilishi wa mtandao wa Instagram kuacha kazi kutoka kwenye kampuni yake.
Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi juu ya nani atakaye shikilia nafasi za wabunifu hao baada ya wabunifu hao kuachana na mtandao huo ndani ya wiki mbili zinazokuja ila kwa taarifa zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Swahili Tech kila siku.
Idadi ya watumiaji wa teknolojia inazidi kupanda kila siku, vilevile kwa sababu ya kukuwa kwa teknolojia wengi ya watu hawa sasa wanahitaji kufanya manunuzi mtandaoni, pamoja na hayo wote tunajua usumbufu unaoweza kuupata ili kupata kadi ya benki yenye kuweza kufanya manununzi mtandaoni, ndio maana kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Mastercard inaleta huduma nzuri sana na rahisi ya kufanya manunuzi mtandaoni ya M Pesa Card.
M Pesa Card hii ni huduma mpya kutoka Vodacom ambayo itakuwezesha kupata kadi yako ambayo utaweza kuitumia kufanya manunuzi mtandaoni kwa haraka bila kuwa na haja ya kwenda benk au mahali popote kujisajili na huduma hiyo.


Sasa kama tayari unajua kuhusu huduma hii basi na uhakika tayari umeshaweza kujiunga, ila kama ufahamu basi unaweza kufuata maelezo haya, Kama unatumia laini ya simu ya Vodacom, unatakiwa kubofya namba za M Pesa ambazo ni *150*00#, baada ya hapo chagua Menu namba 4 ambayo imeandikwa Lipa kwa M-Pesa, baada ya hapo chagua namba 6 ambayo imeandikwa M-Pesa Mastercard baada ya hapo kama hii ni mara yako ya kwanza kutumia huduma hii unatakiwa kuchagua namba 1 ambayo imeandikwa Tengeneza Kadi.
Baada ya kutengeneza kadi utaletewa ujumbe mfupi wa maneno wenye tarehe ya kuisha kwa matumizi ya kadi au Expiry, namba ya utambulisho wa kadi au Card number yenye tarakimu tisa, pamoja na CVV yenye tarakimu tatu. Mambo yote haya ni muhimu sana pale utakapo taka kufanya manunuzi mtandaoni hivyo hakikisha unahifadhi meseji hiyo kwaajili ya matumizi ya haraka.
Sasa kukupa ufafanuzi kidogo ni kuwa, namba hizo zilizopo kwenye meseji hiyo ndio M-Pesa Card, hiyo ni Virtual Card au tuseme kadi ya kidigitali ambayo sio ile ya kushikika ambayo unapewa benki, bali hii ni kadi ambayo unaweza kuitumia bila kuwa na kadi ile ya plastiki, na matumizi yake ni sawa kabisa na kadi ya kawaida yenye uwezo wa kufanya manunuzi mtandaoni.
Kumbuka pale unapotaka kufanya manunuzi unatakiwa kujua namba hizo na hakikisha unaweka pesa kwenye kadi yako kwa kuingia kwenye menu ya M-Pesa kisha chagua 4 kisha chagua 6 alafu chagua namba 3 ambayo imeandikwa weka pesa kwenye kadi, kisha ingiza kiasi kisha subiri kidogo utaletewa meseji yenye kukutaka kudhibitisha kwa kubofya 1 au kubatilisha kwa kubofya 2, baada ya hapo kama umethibitisha utaletewa sehemu ya kuandika password yako ya M-Pesa na baada ya muda kidogo utakuwa umamaliza kuweka hela na utaletewa ujumbe kuwa pesa imewekwa kwenye kadi yako.
Baada ya hapo sasa utaweza kufanya manunuzi mtandaoni kwa urahisi na haraka. Ukweli huduma hii inarahisisha mambo mengi sana kwa watanzania hivyo ni matumaini yangu sasa huduma nyingi zitaweza kulipiwa kutokana na kuwezeshwa kwa huduma hii.